Mkulima wa Pareto kutoka Igoma wilaya ya Mbeya William Mwakatobe akielezea tatizo la wakulima kukopwa maua ya pareto na kucheleweshewa malipo yao ya pili |
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Wadau wa Pareto Lawrence Tara akifafanua jambo katika kikao cha Wadau wa Pareto mjini Makambako Njombe |
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Awariywa Nnko akichangia hoja katika kikao cha Wadau wa Pareto Makambako |
Mkurugenzi wa Bodi ya Pareto Ephraim Mhekwa akitoa ufafanuazi katika kikao cha Wadau wa Pareto kilichofanyika Makambako mkoani Njombe mwishoni mwa wiki. |
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe imedai kuwa wanunuzi wa zao la Pareto
wamekuwa wakikwepa ushuru kwa kununua zao hilo nyakati za usiku na kutoroka
bila kulipa ushuru wa Halmashauri hiyo.
Hayo
yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Jison
Mbalizi alipokuwa akichangia hoja kwenye kikao cha Wadau wa zao la Pareto
kwenye Ukumbi wa Mid Town mjini Makambako mwishoni mwa wiki.
‘’Wanunuzi
wanaingia Makete kinyemela nyakati za usiku na kununua pareto bila kulipa
ushuru wa Halmashauri, huo ni wizi, tunaomba hatua zichukuliwe dhidi ya
makampuni hayo,’’alisema Mbalizi.
Alisema kuwa
Halmashauri haijalipwa ushuru kwa zaidi ya miezi sita huku kampuni zikiendelea
kununua pareto ana kwamba kuna haja ya kudhibiti hali hiyo ambayo inapunguza
mapato ya halmashauri yatokanayo na ushuru wa mazao.
Naye mkazi
wa kijiji cha Tembela wilaya ya Mbeya William Mwakatobe alisema kuwa Bodi ya
Pareto inapaswa kuangalia taratibu za wanunuzi ambao wanadhulumu haki za
wakulima na kusema kuwa wakulima wamekuwa wakikopwa maua ya pareto na kugoma
kulipa malipo ya pili.
Mwakatobe
alisema kuwa kinachofanywa na kampuni ya ununuzi wa pareto ni kuchukua maua ya
pareto kwa mkopo bila kulipa hivyo kusababisha wakulima wa zao hilo kutoona
umuhimu wa kuendelea kulima zao hilo.
Kwa upande
wake Meneja wa Kampuni ya PCT inayonunua Pareto wilayani Makete, Martin Oweka
alisema kuwa kampuni yake itafanya jitihada za kulipa deni inalodaiwa na kwamba
lipo tatizo kwa mawakala wao katika wilaya za
Makete,Mbeya Vijijini,Ileje, Mufindi na Kilolo.
Oweka
alisema kuwa tatizo hilo(hakulifafanua) limesababisha kuwa na madeni kwa
wakulima na kuwa hata hivyo watalipa madeni hayo baada ya mchanganuo muda mfupi
ujao.
‘’Sio sera
yetu kukopa, tunalipa kulingana na takwimu, tunapeleka fedha kila wiki
inaonesha mawakala wetu ndio tatizo,’’alisema Oweka.
Kwa upande
wake Mwanasheria kutoa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Shani Mayosa
alisema kuwa kutolipa wakulima na kukwepa ushuru ni kosa na kwamba si jambo la
busara kuendelea kutoa leseni ya biashara kwa wanunuzi ambao hawana manufaa kwa
wakulima.
Aidha Mkurugenzi
wa Bodi ya Pareto Ephraim Mhekwa alisema kuwa wanunuzi wanapaswa kuzingatia
ubora wa zao hilo ili kukidhi viwango vya Kimataifa na kuwa serikali imeweka
mkakati wa kuanza kuchoma maua ya pareto yasiyokidhi viwango ili kuwa na
nidhamu ya kilimo bora cha Pareto nchini.
Hello dear mwombaji Mimi ni Mheshimiwa Stephen Brown kwa jina na i ni mmiliki wa Trust Fedha World Loan Company. Kwa heshima ya matendo yangu kubwa, mimi itabidi kama wewe kujua kwamba i kutoa kila aina ya mkopo unaweza milele kufikiria katika tu kiwango cha riba ya 3%. Harakisha sasa na kuomba kwa ajili ya mkopo wako haraka ili tuweze kupata mkopo wako mbio. Wasiliana nasi leo saa: trustfunds402@yahoo.com Omba kwa ajili ya mkopo wako leo na kupata hivyo kwa haraka kama unataka hivyo. * STEPHEN BROWN *
ReplyDelete