Mkuu wa wilaya ya Momba Abihudi Saideya akisisitiza jambo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Momba. |
Diwani wa Viti Maalum kata ya Ivuna Colletha Mwaselela aliyeibua hoja ya kushambuliwa kwa Ufuta na wadudu wa ajabu. |
Kaimu Ofisa Kilimo wa wilaya ya Momba Henry Kiondo |
Vijiji
vilivyoathiriwa na janga hilo na majina ya kata zake kwenye mabano ni
Mkongo,Usoche, Senga na Muuyu(Kamsamba),Vijiji vya Mkulwe,Namsinde na
Itelesya(Mkulwe) na vijiji vya Ivuna, Ifumbula,Samang’ombe na Mkomba(Ivuna).
Kwa mujibu
wa wakulima wa zao hilo walidai kuwa wadudu hao wenye ukubwa mithili ya mchanga
wanafanana na viwavi wanapokuwa wadogo na baadaye huwa kama Panzi wadogo ambao
hukaa ndani ya maua ya Ufuta kabla ya kupasuka.
Wadudu hao
wamedaiwa kushambulia mazao hayo kwa kipindi cha miaka miwili mfulululizo
ambapo awali wakulima wa vijiji hivyo walizoea kulima bila kutumia mbolea
wala dawa za kuulia wadudu.
Mmoja wa
wakulima wa zao hilo ambaye ni Diwani wa Viti maalumu kata ya Ivuna Colletha
Mwaselela alisema kuwa yeye aliwekeza kwenye shamba lenye hekari 15
kiasi cha sh. milioni 3.5 na matarajio yake ni kupata debe 400
ambazo angeuza kwa sh. Milioni 18 lakini alivuna jumla ya debe 62 alizopata
kiasi cha sh. Milioni 2.8.
Naye
Diwani wa Kata ya Kamsamba Hezrone Sapali alisema kuwa yeye alilima kiasi cha
hekari 11 ambazo aliwekeza kiasi cha sh. Milioni 1 kwa matarajio ya kupata
jumla ya sh. milioni 4 lakini alivuna kiasi cha debe 52 alizouza sh. milioni 1.
Mkulima
mwingine ambaye ni Diwani wa Kata ya Mkulwe Mathew Chikoti alisema kuwa yeye
alilima jumla ya hekari 10, lakini alivuna hekari 5 tu na zingine
zilishambuliwa na wadudu na hivyo kujikuta akipata hasara na kuwa aliwekeza
jumla ya sh. 1.5 na matokeo yake alipata chini ya matarajio kiasi cha
sh.milioni 1.
Kwa upande
wake mkulima mkazi wa kijiji cha Karungu kata ya Ivuna Gervas Zyembele alisema
kuwa alilima jumla ya hekari 48 ambazo alitarajia kuvuna kiasi cha gunia 100
ambazo angeuza jumla ya sh. milioni 35 lakini amevuna debe 48 ambazo ameza
jumla ya sh.milioni 1.4.
Zyembele
aliiomba serikali kutembelea kwa wakulima kujua matatizo yaliyosababisha zao
hilo kushambuliwa na wadudu hao.
Kaimu
Ofisa Kilimo wilaya ya Momba Henry Kiondo alisema kuwa tatizo hilo
limetokana na wakulima wengi kutojua mchanganyiko wa dawa za kuulia wadudu na
kuwa eneo hilo walizoea kulima bila kutumia dawa wala mbolea.
Alisema
kuwa dawa za zao la ufuta ni ghali na kuwa wakulima wengi hawamudu kununua dawa
na kwamba ni vyema wakulima wakafuata ushauri wa kilimo bora cha ufuta ikiwa ni
pamoja na kutolima kwenye maeneo yenye maji mengi.
Mkuu wa Wilaya ya Momba Abihudi Saideya alisema
kuwa hajapata rasmi taarifa hizo na kuwa hata hivyo amewataka watendaji
wa Idara ya Kilimo kufuatilia tatizo hilo na kutoa elimu kwa wakulima ili
tatizo hilo lisijirudie katika msimu ujao.
Post a Comment