Sina Baba
wala Mama, naishi na bibi yangu mzaa mama simjui baba yangu, mama yangu
alifariki, sisomi shule, sina madaftari wala nguo za shule,nachunga ng’ombe wa
jirani yetu, bibi yangu ni mkulima, tunapata chakula kwa kubangaiza, siku
nyingine tunalala na njaa, bibi yangu ni mzee sana.
Ni kauli ya mtoto
huyu(aliyejitambulisha kwangu jina lake)anayefikia umri wa miaka 12 mkazi wa
kijiji cha wavuvi na wafugaji (katika
eneo hili nililotembelea)ambaye kwa kawaida alipaswa kuwa shuleni akipata elimu.
Familia
nyingi za maeneo ya vijijini zimekuwa katika kadhia za aina hii, maisha ya
sulubu ndiyo waliyoyazoea, wameyakubali na kuyafanya kuwa ni sehemu ya maisha
yao ya kila siku.
Ni nadra kwa
mtu wa kawaida kuyazoea maisha ya aina hii lakini ipo jamii ambayo imelazimika
kuyakubali na kuyapokea maisha haya na kuyafanya kuwa ni sehemu ya maisha yao
ya kawaida.
Ni vigumu
kuizoea hali hii lakini haya ndiyo maisha ambayo jamii hii imeyazoea na
kuyakubali aghalabu familia nyingi za mjini huishi maisha yenye nafuu ingawa
pia huikumbana na dharuba za kila siku za kuishi chini ya dola moja, ni tabaka
la watu wa kawaida, nao wameyazoea na kuyakubali maisha ya aina hii.
Unaweza
kuyakubali au kuyakataa maisha ya iana haya lakini mazingira halisi ya kipato
yanakushawishi uyakubali na uishi katika hali hiyo kwa kadri ambavyo Mungu
amekujaalia.
Kilio cha
jamii hii kinapaswa kuelekezwa wapi? Katika jamii yenyewe au kwa washika
dhamana kwenye mhimili mkuu, walioshika mpini wakawapa makali walalahoi ili
wagombanie kukatwa mikono yao.
Post a Comment