Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa mkoa wa Mbeya wakifuatilia maadhimisho ya kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya kanisa la TAG |
Rais Jakaya Kikwete akifuatilia kwa makini sherehe za miaka 75 ya kanisa la TAG katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jana(kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro. |
Baadhi ya Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakichukua matukio wakati wa kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya kanisa la TAG katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya. |
RAIS Jakaya
Kikwete amevunja ukimya juu ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba mpya na kuomba
usadizi kwa viongozi wa dini kusaidia kuombea Umoja ya Katiba ya Wananchi (UKAWA)kurejea
katika mjadala a Bunge la Katiba ili hatimaye ipatikane katiba itakayokidhi
matakwa ya Watanzania.
Akizungumza
katika kilele cha Jubilei ya miaka 75 ya Kanisa la Tanzania Asembless Of God
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jana Rais Kikwete alionesha hofu yake ya
kutokamilika mchakato wa kuundwa kwa Katiba hiyo iwapo UKAWA hawatarejea bungeni.
‘’Mjadala wa
katiba ulianza vizuri walikubaliana kulingana na kanuni zao kuunda kamati 12,
mjadala wa sura ya ya 1 na 2 ulichukua siku 19 badala ya siku 14 April 10 bunge
lilikutana, April 13 taarifa zote
ziliwasilishwa, April 16 wajumbe wa CUF, CHADEMA na NCCR Mageuzi walitoka nje,’’alisema
na kuongeza.
‘’Tena hawa
ndugu zetu walitoka nje bila kuweka masharti ya kurejea kwamba kikifanyika hiki
au kile watalegeza masharti yao, hawakutoa masharti ya kurudi, sisi matumaini
yetu wote warudi ili wafanye maamuzi kwa pamoja,’’alisema Rais Kikwete.
Alisisitiza
kuwa swala la kurudi ama kutorudi bungeni haliwatatizi viongozi wa dini pekee
bali hata yeye binafsi na kwamba kuna haja ya viongozi wa dini kutumia nafasi
yao kuwaombe wanaosababisha mgongano katika jamii ya Watanzania.
‘’Kama kuna
mapepo ya kuombea, TAG mtuombee hili pepo la kutoelewana liondoke, wameanza
mchakato kamati zote 12 zimekamilika kwenye mjadala wa jumla mapepo yakaingia, huyu kamsema huyu na Yule kamsema
mwingine, kama kuna mapepo waheshimwa hawa waombewe warudi wasafiane nia,’’aliendelea
kusihi Rais Kikwete.
Hata hivyo
Rais Kikwete alisema kuwa ameanza kupata matumaini baada ya Msajili wa Vyama
vya Siasa Jaji Mstaafu Francis Mutungi amefanya jitihada za kuwakutanisha
viongozi wa vyama vikuu vinne vya siasa ambao wanaendelea mjadala juu ya hatima
ya katiba.
‘’Batati nzuri
wawakilishi wa CCM,CUF,CHADEMA na NCCR Mageuzi wanakutana, watokaje hapa ili
waende mbele, nawapongeza viongozi wa vyama hivi, pia natoa pongezi maalum kwa
Msajili wa vyama Jaji Mutungi, naamini hivi vyama vikubwa vinne vikikubaliana
mambo yataenda.’’alisema.
Aidha
aliwasihi wananchi kuwaachia nafasi viongozi hawa waendelee na mjadala wao bila
kuingiziwa maneno mengine ambayo yatawakatisha tamaa bali wanatakiwa kupewa
moyo.
‘’Watanzania
wenzangu hebu tuwape nafasi hawa wajadili, kwa utulivu, tusiwachanganye,zaidi
tunapaswa kuwaombea, miluzi mingi inampoteza mbwa usasi, unajua mbwa akipigiwa
miluzi wakati wa kuwinda hawezi kwenda atasimama,’’alisema.
Rais Kikwete
alishangazwa na baadhi ya watu ambao wanafanya kazi ya kupoteza umma kila jambo
jema linapofanyika na kuonya kuwa iwapo kuna watu wamechukua zabuni ya kuwalipa wanaoendeleza
tabia hiyo ili serikali ifidie gharama za vitendo vyao.
‘’Wengine
kazi yao ni kuongopa tu sijui tenda hii wanalipwa na nani kusema uongo, sisi
serikali tutamlipa ili aache tenda hii ya kuvuruga watu, kazi yao ni kuvuruga
watu wasielewane, hivi hili linatoka wapi, mwisho wa siku mtapandikiziana chuki
na kuuana bure,’’alionya.
Awali
akizungumza katika maadhimisho hayo Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Asembless
Of God (TAG) Dkt.Barnabas Mtokambali aliwaomba wajumbe wa Bunge Maalum la
Katiba ambao wamesusia vikao vya Bunge hilo kurejea katika majadiliano ili iweze
kupatikana katiba mpya itakayotoa mustakabali wa nchi yetu.
Alisema
viongozi wa dini wamekuwa mstari wa mbele kuombea amani ya nchi na kuwa vitendo
vya wajumbe wa Bunge la Katiba kususia vikao vya bunge hilo vinawakatisha tamaa
wananchi na hivyo kukosa imani ya kuwa na Katiba itakayokidhi matakwa ya
wananchi wote.
Post a Comment