wataalam wa sekta ya kilimo kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mlele wakikagua mashamba Kijiji cha Mwamapuli Katika Bonde la ziwa Rukwa ambalo ni eneo maarufu kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali. |
Na Kibada Kibada
–Katavi.
Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele mkoani Katavi imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 868.3 sawa
na asilimia ya 72 ya lengo liliowekwa la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni
1.2 kwa kipindi cha mwezi julai 2013 hadi kufikia juni 2014.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya fedha ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Wilbrod Mayala kwenye kikao cha Baraza la
Madiwani ilieleza kuwa Halmashauri ilijiwekea lengo la kukusanya kiasi
cha shilingi bilioni 1,214,078,000/=.
Mwenyekiti huyo alieleza
kuwa hadi kufikia kipindi hicho Halmashauri ilikuwa imefanikiwa kukusanya jumla
ya kiasi cha shilingi 868,383,958.46 ambayo ni sawa na asilimia 72.
Alieleza kuwa Mapato
hayo yanatokana na vyanzo mbalimbali ambavyo ni Ruzuku ya Kawaida,Vyanzo vya
ndani,Fidia ya vyanzo vingine vilivyofutwa na serikali,Pamoja na mifuko
mbalimbali ya miradi ya maendeleo.
Akizungumzia matumizi
alielezakuwa Halmashauri ililenga kutumia jumla ya shilingi 565,518,205.25 hata
hivyo matumizi halisi yalikuwa kiasi cha shilingi milioni 819,304,922.34
sawa na asilimia 145 hivyo kuvuka makusanyo waliyokusanya.
Akizungumzia mipango
mikakati iliyowekwa kwa ajili ya kuongeza ukusanyaji wa mapato alieleza kuwa
wameweka mikakati ya kufungua barabara ya Mwamapuli hadi majimoto kupitia
mwamatiga ili kurahisisha usafiri na usafirishaji na kuongeza mapato ya
makusanyo.
Mikakati mingine ni
kukitangaza kituo cha Mwamapuli ambacho kinahusika na Masuala ya Habari za
Kilimo ili kukutangaza nje ya mipaka ya Mkoa wa Katavi kwa ajili ya kuvutia
wawekezaji kwa kueleza hali halisi ya uzalishaji wa zao la mpunga katika wilaya
ya Mlele ili kukaribisha wawekezaji kuja kuwekeza zaidi katika maeneo hao ya
sekta ya kilimo.
Mikakati mingine ni
kupeleka maombi ya fedha US-AID kwa mwaka huu 2014 kuombea fedha kwa
ajili ya kujenga skimu ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji .
Post a Comment