Huyu ni mtoto wa Kitanzania ameduwaa hapa porini anatafakari maisha yake anahitaji elimu bora anahaha hajui aanzie wapi nini mustakabali wa maisha yake.. |
akiwa na kundi la ng'ombe kuanzia alfajiri hadi usiku. akipata njaa hula matunda na kurejea nyumbani jioni |
Haya ni makazi ambayo kijana huyo mchungaji wa ng'ombe hurejea jioni na kesho yake huamka mapema kwenda machungani |
Eneo hili ndio kidogo lenye unafuu wa maisha ambako angalau kuna nyumba chache zilizoezekwa kwa bati hata hivyo umbali kutoka hapa hadi ilipo shule ya msingi huwafanya watoto waogope kwenda shule.. |
Mara kadhaa wanafunzi hujikuta wakiwa kisiwani baada ya mvua kunyesha na kushindwa kuvuka kuwahi masomo |
Wengine hupata msaada wa kuvushwa kwa kubebwa migongoni kama inavyoonekana hapa lakini mara kadhaa watoto hawa hujikuta wakiwa wamechelewa masomo |
dah inasikitisha jamani hata sijui naweza kutoa mchango gani ila kwa staili hiyo hawawezi kufanikiwa katika masomo yao maana ni mazingira magumu sana kwa kweli
ReplyDelete