Ads (728x90)

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa enzi za uhai wake
Mapema leo zilipatikana taarifa za kuanguka kwa mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Tarime John Henjewele alipokuwa katika ziara ya kikazi wilayani humo.
Taarifa za awali zilizosambazwa katika vyombo vya habari vilisema kuwa Mkuu huyo wa mkoa alianguka ghafla na kuanza kutoka povu mdomoni na baadaye alikimbizwa katika hospitali ya wilaya kwa ajili ya matibabu.
Lakini taarifa zilizotujia baadaye zilielezwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa amefariki dunia majira ya saa 5 asubuhi  katika Hospitali ya wilaya ya Tarime, baada ya kuanguka ghafla na kutokwa na povu wakati akitoka nje ya ofisi ya Mkuu wa Wilaya (DC) Tarime.

Baada ya tukio hilo, Mkuu wa Mkoa huyo alikimbizwa hospitalini na akafariki dunia muda mfupi wakati timu ya madaktari wa hospitali hiyo ikijiendelea na harakati za kunusuru maisha yake.

Mmoja wa watu waliokuwa jirani na kiongozi huyo, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita alisema “nina mfahamu marehemu na naweza kusema alikuwa ni mwalimu wangu bingwa wakati nikiwa Dodoma.”

Huku akitokwa na machozi kwa mbali, Guninita alisema ameguswa na kifo cha kiongozi huyo aliyekuwa akitegemewa na familia yake na maendeleo ya Taifa.
Mungu ametoa, Mungu ametwa, jina la Mungu lihimidiwe

Post a Comment