Ads (728x90)

Kikundi cha sanaa cha nyimbo za Asili cha Wane Star kilitoa burudani kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari MCT Kajubi Mukajanga akisoma hotuba kabla ya utoaji wa Tuzo na zawadi kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013
Baadhi ya wanahabari wakiwa na Tuzo na zawadi  Umahiri wa Uandishi wa Habari wakishangilia ushindi mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari nchini (MCT) Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa wanahabari 76 walioshiriki katika tuzo ya umahiri wa uandishi bora nchini.

Baadhi ya wanahabari wakishiriki katika hafla ya utoaji tuzo na zawadi kwa waandishi wa habari bora nchini.


Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Joseph Kulangwa akishangilia jambo wakati wa utoaji wa tuzo za Umahiri wa Uandishi Bora nchini

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Joseph Kulangwa akimpongeza mwandishi wa habari wa gazeti hilo Khadija Mussa aliyeshinda tuzo ya habari za uandishi wa Utawala Bora
Mwandishi wa habari Mwandamizi Manyerere Jacton wa Jamhuri na Paul Mabuga wa Star TV wakifuahia jambo katika ukumbi wa Mlimani City muda mfupi kabla ya kuanza rasmi kwa utoaji zawadi kwa wanahabari mahiri wa mwaka 2013
Watendaji wa Baraza la Habari nchini MCT, Kajubi Mukajanga, Pili mtambalike, Alan Lawa a wengineo wakiweka mipango ya kukaribisha wageni wakati wa hafla ya utoaji zawadi kwa wanahabari mahiri waliofanya vizuri mwaka 2013
Jaji Mstaafu obert Kisanga akijadili jambo na Rais wa Majaji wa Afrika Mashariki Harold Nsekela huku wakishuhudia waandishi mahiri wakipita jukwaani na kupokea tuzo na zwadi zao
Baadhi ya wahariri na wadau wa vyombo vya habari walipata fursa ya kuwashuhudia wanahabari mahiri kwa kazi za Uandishi wa habari nchini, pichani nguli wa habari za uchunguzi Ndimara Tegambwage akijadili jambo na wadau wa habari.
Wageni kutoka ndani na nje ya nchi walialikwa katika hafla hiyo mahususi kwa wanahabari waliofanya vizuri zaidi katika kazi za habari mwaka 2013
Waandishi walipata fursa ya kuchat huku wakibadilishana mawazo wakisubiri kupata tuzo na zawadi walizoandaliwa na Baraza la Habari nchini (MCT)
Mwandishi wa habari wa ITV na Redio One Festo Sikagonamo akisalimiana na Bosi wake Mkurugenzi wa ITV na Redio One Joyce Mhavile wakati wa utoaji tuzo na zawadi kwa waandishi habari mahiri wa mwaka 2013 nchini.

Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo Joseph Kulangwa akiteta jambo na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya habari MOAT Dkt. Reginald Mengi wakati wa utoaji wa tuzo kwa waandishi wa habari mahiri nchini
Dkt. Mengi akifurahia burudani iliyokuwa ikirendelea katika ukumbi wa Mlimani City wakati wa utoaji tuzo na zawadi kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013
Mwandishi wa habari mwandamizi Abdallah Majura akifurahia a tuzo yake ya habari za Uchunguzi kwa vyombo vya Redio huku Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari Dkt. Mengi akifurahia.
Waandishi wa habari Gordon Kalulunga wa Kalulunga Blog,Frank Leonard wa Bongo Leaks na Mashaka Mgeta wa Gazeti la Mwananchi wakiwa jukwaani wakisubiri kukabidhiwa zawadi na tuzo kwa stori za Afya ya Uzazi na Mimba za utotoni
Mwandishi wa habari kutoka Fasihi Media Ink Rashid Mkwinda akikabidhiwa zawadi kutokana na habari za Mazingira wakati wa utoaji tuzo na zawadi kwa waandishi mahiri wa mwaka 2013, baadhi ya zawadi zilizotolewa ni pamoja na King'amuzi na Dish la DSTV, vyeti,Smart Phone Galaxy,Luninga na Ngao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Kajubi Mukajanga akitoa hotuba kabla ya ugawaji wa Tuzo na Zawadi kwa waandishi wa habari mahiri wa mwaka 2013


Mwandishi wa habari mwenye mafanikio ya maisha katika habari Mariam Hamdan akipongezwa

Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Redio One Joyce Mhavile akisoma wasifu wa mwandishi mahiri mwenye mafanikio katika kazi za Uandishi wa Habari Mariam Hamdan
 Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari MOAT Dkt. Reginald Mengi akimkabidhi luninga Mshindi wa Jumla wa Tuzo za Uandishi wa Habari nchini Idd Juma kutoka Afya Redio ya Jijini Mwanza.
Mchora katuni bora wa mwaka 2013 Muhidin Msamba akiwa na tuzo yake mara baada ya kutangazwa kuwa ni mchora katuni bora nchini
Mwandishi wa Habari wa ITV na Redio One Asraji Mvungi akipokea tuzo za uandishi wa habari bora za Watoto kupitia Luninga
Waandishi wa habari, Isakwisa Mwaifuge, Sam Mahela na Festo Sikagonamo wa ITV walikuwa ni miongoni mwa wanahabari mahiri waliofanikiwa kupata Tuzo na Zawadi mwishoni mwa wiki ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Msanii mahiri wa nyimbo za asili Wane Star akitoa burudani wakati hafala ya utoaji wa utoaji wa zawadi na tuzo kwa wanahabari mahiri nchini.


Post a Comment