Ads (728x90)

Safari yetu  kuelekea Jijini Lilongwe nchini Malawi iliendelea hadi kijiji maarufu  cha Mponela kilichopo katika wilaya ya Kasungu mkoa wa Kati hapa ni eneo maarufu kwa Nyama Choma, ya mbuzi, tulisimama na kupooza njaa kwa kutafuna finyango mbili tatu za Nyama ya Mbuzi kisha tukatelemshia na maji.

Moja ya mambo tofauti tuliyoyaona hapa ni kuwepo kwa baiskeli maalumu za kubeba abiria, maeneo mengi ya miji ya nchini Malawi hakuna matumizi ya Bodaboda wala Bajaj sijui ni kutokana na taratibu za nchi hiyo ama la, bali kama si sheria basi ni fursa pekee kwa wajasiriamali wa Tanzania kufikiria kuwekeza nchini humo.


Mmoja wa moderator wa Mbeya Yetu wamiliki wa Blog za Mikoa Fred Njeje akiwa katika pozi kwenye moja ya baiskeli ambazo hutumika kusafirisha abiria nchini Malawi.Kati ya mambo mapya niliyoyaona ni hali kama hii, jamaa amembeba mbuzi kwa mtindo wa aina yake akimpeleka kuuza kwa ajili ya watu kuchinja na kujipatia asusa, kumbuka eneo hili la Mponela ni maarufu kwa Mbuzi Choma.


Jiji la Lilongwe lilianza kuonekana baadhi ya mitaa yake tunapoingia mjini.

Tuliwasili Lilongwe majira ya saa 12:30  sawa na saa moja  na nusu ya Tanzania tukapokelewa na mwenyeji wetu katika Hotel ya Sabina, mahala ilipo Hotel hii ni maarufu sana kwa Watanzania na ndipo ambapo ni karibu na Stendi Kuu ya Mabasi yanayotoka nje ya nchi, tuliona Ofisi ya mabasi ya TAQWA hapa unaweza kukutana na mtu ukaongea naye lugha ya Kiswahili.

Tulikutana na mwenyeji wetu mwandishi wa habari wa Malawi Francis Tayanja Phiri akatulaki kwa furaha na kutukaribisha yeye alisafiri kutokea Blantyre na kuingia Lilongwe dakika 20 zilizopita.

Rais Mstaafu wa Shirikisho la Vilabu vya Waandishi wa Habari nchini Tanzania(UTPC) Ulimboka Mwakilili akisalimiana na Mwandishi wa habari nguli wa Malawi Francis Tayanja walipokutana Jijini Lilongwe, Malawi kwenye ziara ya waandishi wa habari wa Tanzania nchini humo.

Mwandishi wa habari mwandamizi nchini Tanzania anayeandikia kampuni ya Free Media Christopher Nyenyembe akisalimiana na Mwandishi mkongwe wa nchini Malawi anayeandikia magazeti ya Kampuni ya Blantyre News Paper mara walipokutana Jijini Lilongwe nchini Malawi.


Mwandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Raia Mwema Felix Mwakyembe akisalimiana na nguli wa habari nchini Malawi Francis Tayanja Phiri Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Ilikuwa ni furaha kubwa kukutana na mwenyeji wetu mara tukaanza kubadilishana mawazo na kupeana taarifa za safari yetu ndefu kutokea nchini Tanzania, kupitia Karonga, Mzuzu hadi Lilongwe.

Mwandishi wa habari Francis Tayanja Phiri akitoa taarifa fupi ya ratiba ya siku inayofuata kwa waandishi wa habari kutokea nchini Tanzania.
Baada ya kikao cha muda mfupi tulikutana kwa ajili ya chakula cha jioni katika Hoteli moja iliyopo jirani na mahala tulipofikia.


Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Brandy Nelson akitahayari na kutafakari juu ya aina ya maisha waishio majirani zetu wa nchini Malawi, hapa ilikuwa ni katika Klabu ya Usiku.


Brandy Nelson mwandishi wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania


Fred Njeje Moderator wa Mbeya Yetu Blog na Blog za Mikoa akijivinjari katika Klabu ya usiku Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Post a Comment