Ads (728x90)

Hapa ni Taifa Market Jijini Mzuzu maarufu kwa Watanzania wengi hufanya shughuli zao ni eneo ambalo unaweza angalau kujivunia kwa kukutana na watu wa nyumbani,wanmaozungumza lugha ya nyumbani ni Jiji safi lililowekewa miundo mbinu safi na hapa niliposimama ni ghba la takataka kila baada ya muda gari la kuzoa taka hupita hakuna vumbi kama tulilozoea nyumbani, unaona aibu hata kutupa chini vocha uliyokwangua na kuweka katika simu yako.

Katika eneo maalumu Jijini Mzuzu panaitwa Mzuzu Coffee Den hapa ukiingia kuna Wire Less Internet, unanunua muda wa hewani kisha unaunganishwa kwa wireless kwenye Laptop yako unafanya kazi kwa saa tatu kwa kulipa kwacha 500 hii ni sawa na shilingi za kitanzania elfu 2000Tulipata muda mzuri wa kufile stori zetu kupeleka kwenye vyombo vyetu nchini Tanzania kwa kuwa network ilikuwa inasumbua kutokana na kubadilisha line za nchini kwetu hadi ufanye roaming na kutozowea kutumia mitandao ya nchi ya watu tukashindwa kutuma stori tukiwa katika Hotel tuliyofikia.
 

Ndani ya Mzuzu Coffee Den Jijini Mzuzu nchini Malawi

Post a Comment