Ads (728x90)

Jijini Mzuzu tuliagwa na kupewa baraka na Rais wa Nyika Media Club Chimbizga Msimuko  kututakia safari njema kuelekea Jijini Lilongwe, safari yetu ilianza tukaingia ndani ya magari yetu matatu kila gari tulipanda watu wanne tulisafiri kwa raha mustarehe bila bughudha.
Njiani tulishuhudia namna ambavyo Mwenyezi Mungu alivyoumba dunia kwa kuweka milima iliyofanana na vigingi vilivyosimikwa ardhini kuisimamisha dunia.

 

Tulisafiri kwa mwenda mrefu tukasimama kuchimba dawa katika baadhi ya nyumba katika kijiji kimoja cha Luwawa wilayani Mzimba mkoa wa Kaskazini.

Kama ilivyo kwa wanavijiji wa Tanzania hapa pia wapo wanavijiji wanaoshabihiana kwa mila na desturi, Mary Nkhoma ni mama mwanakijiji wa Luwawa alikuwa akiandaa chakula cha mchana kwa ajili ya familia yake, alikuwa kipiga ugali,wenzetu wa nchini Malawi wamezoea kula ugaali laini unaoliwa kwa vidole tofauti na nchini Tanzania ugali lazima uufinyange kwa kiganja chote na kuutumbukiza kinywani. ugali unaotokana na mahindi a unaopikwa Malawi ni laini,unapikwa na kuliwa kwa mboga yoyote.
  



Baadhi ya nyumba za maeneo haya kijiji cha Luwawa WILAYA ya Mzimba nchini Malawi ni sawa na baadhi ya nyumba za vijiji vya TANZANIA


Tulivutiwa na uchomaaji wa mbuzi kwa njia ya kukaanga kwenye karai tulitafuna nyama ya mbuzi kutuliza njaa


Wamiliki wa Mbeya Yetu hawakuwa nyuma kupata picha mbalimbali za matukio na wenyeji wa kijiji hiki cha Luwawa, tyatizo pekee tulilokutana nalo maeneo mengi wakazi wa maeneo haya hawajui Kiingereza wala kiswahili hivyo ilituwia vigumu, kuelewana mahala pengine tulitumia lugha za ishara ili kupata mawasiliano.


Tulifika katika mji maarufu wa Jenda hapo tulipata fursa ya kupumzika kidogo, ni safari ya kuelekea Jijini Lilongwe, ilikuwa ni safari nzuri ya kuvutia.

Tulikutana na baadhi ya vijana kama ilivyo kwa vijana wa Kitanzania maeneo ya vijijini hapa vijana wakifurahia uwepo wetu mahala hapo na kuomba kupigwa picha hasa walipoona tisheti zetu zimeandikwa na kuwa na bendera ya TAIFA LETU na kujua tumetokea nchini TANZANIA.

Jambo la kipekee ambalo lilikuwa ni geni kwa upande wetu ni kuona namna vijana wa maeneo ya vijijini wakiuza ndege waliobanikwa na kutungwa kwenye misongo ya vijiti kama mishikaki, tulionja na kula kwa kuchovya kwa chumvi na pilipili, ni nyama tamu ya ndege.

 



Post a Comment