| Tulibadilishana mawazo tukiwa ugenini nchini Malawi kuna wakati tulianza kukumbuka nyumbani |
| Hatukula chakula peke yetu bali watoto tuliokutana nao njiani nao walifaidika na chakula tulichoandaa, walifurahia mlo huo na kutushukuru kwa lugha ya kwao ZIPOMA KWA MBILI |
| Kwa kweli ilikuwa ni baraka kuu ya safari yetu kutoka kwa watoto hao, mratibu wa safari Venance Matinya alikuwa akiwagawia watoto hao chakula, i njia nzima tulisafiri kwa raha mustarehe |
| Ilikuwa ni furaha ya aina yake kuwepo ugenini bila kikwazo chochote njiani |
| Hakuna mmoja kati yetu aliyepata matatizo yoyote katika safari yetu, hakuna aliyeugua kichwa wala mafua sote tulikuwa salama katika safari yetu ndefu. |
| Tuliliacha Ziwa Nyasa na kuendelea na safari yetu!!!! |
Post a Comment