Wanahabari wa Chama Cha waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji wakioneshana Nyani adimu aina ya Kipunji kwenye msitu wa hifadhi ya mlima Rungwe walipotembelea hivi karibuni |
Nyani Kipunji akiwa juu ya mti |
Safari ya kumsaka Nyani Kipunji iliendelea |
Geti kuu la kuingilia kuanza kupandisha mlima Rungwe |
Baadhi ya miti ya asili iliyopo kwenye Hifadhi ya Mlima Rungwe |
Hii ni Camping Site ambayo ilipewa heshima ya jina la Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye alifika hadi hapo na kuzungumza na wahifadhi wa mlima Rungwe |
Ndani ya msitu huo kulikuwa na miti mikubwa na mikongwe |
Maeneo mengi iliwalazimu wanahabari kutafutiza njia kwa kujipenyeza katikati ya miti ili kumsaka Nyani Kipunji |
Mwisho wa safari kila mtu alichoka kiu na njaa ilikatwa kwa kunywa juice na mikate ya asili maarufu kama mabumunda ambayo kiuhakika yalikata njaa ya kurejesha nguvu kama awali |
NI safari ya
ndani ya msitu mnene uliosheheni miti mikubwa ya asili inayokadiriwa kuwa na
umri wa maelfu ya miaka, yenye majani ya rangi ya kijani kibichi kitokanacho na
uoto wa asili uliopo chini ya hifadhi ya Mazingira asilia ya Mlima Rungwe, ukimya uliotawala ndani ya msitu huo,
ubaridi na giza lililotokana na msitu huo kutanda eneo lote la mlima huo uliogopesha na kutia
hofu.
Wanyama
ndege na wadudu wa kila aina walianza kuonekana kuanzia mwanzo wa safari
kupitia geti kuu la Syukula hadi eneo la kilele cha mlima wa hifadhi ya mlima
wa msitu wa Rungwe
wapekee ndio
waliojivunia makazi hayo ambapo milio yao ilionesha aina ya furaha waliyonayo
kuishi katika msitu wa aina hiyo ambao umeendelea kutunzwa na kuhifadhiwa vyema
na serikali.
Hali hiyo
iliwashawishi wanahabari wa chama cha waandishi wa habari za Utalii na
Uwekezaji Tanzania, (TAJATI)wamefanya ziara ya kiutalii kwenye Msitu wa Hifadhi
Mazingira Asilia wa mlima Rungwe wenye ukubwa wa hekta 13,652.1 kwa nia ya kumsaka mnyama adimu duniani Nyani
Kipunji.
Kwa mujibu
wa mhifadhi mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Innocent Lupembe
alisema kuwa Nyani Kipunji ni moja kati ya vivutio pekee vya utalii duniani
ambaye hapatikani kokote zaidi ya msitu huo.
Alisema kuwa
msitu huo umefanywa kuwa ni msitu wa hifadhi wa mazingira asili wa mlima Rungwe
ambako ndani yake kuna baadhi ya wanyama kama vile Mbega,Ngedere. Tumbili na
Nyani aina ya Kipunji ambaye ana asili ya aibu na kupatikana kwake
Alisema lengo
la serikali kuhifadhi msitu huo ni
kulinda Bionuai na rasilimali zilizopo katika msitu huo ambao awali ulikuwa
chini ya usimamiziwa Idara ya Misitu na Nyuki ambapo hata hivyo ulikuwa
unaharibiwa na kuvamiwa na wananchi wanaolizunguka eneo hilo.
Lupembe
alisema kuwa mbali ya kuhifadhi uoto wa asili uliogawanyika kwa sehemu 5 hadi 6
msitu huo una wanyama mbalimbali akiwemo Nyani aina ya Kipunji ambaye
aligunduliwa na Shirika la Kimataifa la Hifadhi ya mazingira na viumbe hai(WCS)
mwaka 2003.
Alibainisha
kuwa hata hivyo ni asilimia 30 tu ya watalii kutoka nje ya nchi wanaotembelea
hifadhi hiyo huku asilimia 70 ni watalii kutoka ndani ya nchi wanaokadiriwa
kufikia watalii 200 hadi 250 kwa mwaka.
Kwa upande
wake Mhifadhi Biolojia wa (WCS) Sophy Machage alisema kuwa msitu huo wa mlima
Rungwe ambao uko juu km 2,981 kutoka usawa wa bahari ni moja kati ya hifadhi za
asili ambayo rasilimali pekee ya Taifa inayohitaji kutunzwa mazingira yake.
Alisema
ndani ya hifadhi hiyo kuna msitu mnene na miti mikubwa ya asili ambaapo chini
yake kuna chemichemi za maji yanayotiririka cjhini kwa chini kuelekea kwenye
mito ya jirani inayopeleka maji Ziwa Nyasa.
Naye
muongoza njia wa mlima huo Mzee Mazao Fungo alisema kuwa eneo la mlima huo
halina njia halisi bali njia zilizopo ni za kubuni kutokana na mazingira ya
msitu na mlima ulivyo.
Alimtaja
Nyani Kipunji kuwa ni mnyama mwenye aibu ambaye kumuona kwake kunahitaji
tahadhari na inawezekana kwa siku mbili au tatu asionekane ingawa kuna wakati
hutembea kwa makundi.
‘’Akisikia kelele
za watu hukimbia kila kundi linakuwa na kiongozi wao mwanaume na mlinzi
wakisikia kelele au mchakacho wa miguu hukaa kimya hata kwa siku nzima
hupendelea kuruka kwenye miti mirefu na huko ndiko makazi yao yalipo’’alisema
Mzee Fungo.
Post a Comment