Kocha wa timu ya Yanga Hans Pluijm akiwa amejishika kichwa baada ya Yanga kuwa nyuma kwa bao 2-1 dhidi ya Prison hadi dakika ya 86. |
Kocha wa Yanga Pluijm akiwa amechanganyikiwa asijue la kufanya baada ya washambuiliaji wa Yanga kukosa magoli mara kadhaa wakiwa wamebaki na golikipa wa Prison ana kwa ana. |
Mshabiki mashuhuri wa Yanga almaarufu Mama Yanga a,kiwa ameanguka baada ya timu yake kufungwa bao la pili na kukimbizwa na gari la wagonjwa Hospitali ya Rufaa Mbeya. |
Mshabiki mashuhuri wa Yanga Ali Yanga akimwangalia mshabiki mwenzie Mama YANGA wakati akipakizwa kwenye gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali ya Rufaa Mbeya. |
Kocha wa Yanga Pluijm akijaribu kuwaelekeza wachezaji wake akiwa kwenye benchi la ufundi la timu yake. |
Kikosi cha timu ya Yanga |
Kikosi cha timu ya Prison |
Almanusura
histroria ya mwaka 2003 ijirejee jana katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine
ambapo timu ya Prison iliwachezesha kwata vijana hao wa mtaa wa Jangwani kwa
mabao 2-0, mabao yaliyofungwa na Paul Mokiwa ambaye kwa sasa ni Afande wa Jeshi
la Magereza mkoani Mbeya.
Katika
mchezo wa jana hali haikuwa kama ilivyotarajiwa ambapo wanajangwani
walishajijengea mazoea ya kujinyakulia pointi zote tatu kila wanapokutana uso
kwa uso na timu ya Prison hali iliyowafanya mashabiki wahisi kuwa timu ya
Prison ni tawi la Yanga.
‘’Prison
anaweza kukaza kwa Simba hata kuifunga ila ikija Yanga haina ubavu wowote
lazima ifungwe hata kama iko kwenye hatari ya kushuka daraja,’’ alisema mmoja
wa mashabiki wa Soka Jijini Mbeya aliyejitambulisha kwa jina la Mwaijande.
Katika
mchezo wa jana kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine Yanga ndiyo iliyokuwa ya
kwanza kupata goli, ikicheza chini ya washambuliaji mahiri akina Donald
Ngoma,Harun Niyonzima,Amis Tambwe,Isoufou Boubacar na Vicent Bossou.
Ilikuwa ni
dakika ya 36 ya mchezo Niyonzima alipoichonga krosi safi upande wa kulia na
kuunganisha mpira uliotua kichwani kwa Tambwe aliyekuwa kwenye boksi na kuusindikiza
mpira wavuni akimuacha golikipa wa Prison Beno Kakolanya akichupa bila
mafanikio.
Hata hivyo
goli hilo la Yanga lilishangiliwa kwa takribani dakika 4 tu ambapo iliamsha
hamasa na munkari wa washambuliaji wa timu ya Prison akina Lambert Sabiyanka,
Freddy Chudu, Mohamed Mkopi na Jeremiah Juma wakilishambulia goli la Yanga kama
nyuki.
Mashambulizi
ya Prison dhidi ya Yanga yalizaa matunda mnano dakika 41 ambapo mchezaji
Jeremiah Juma alifunga bao zuri la kichwa baada ya kuunganishiwa pasi ya
Mohamed Mkopi kutoka upande wa kushoto.
Hadi
mapumziko timu zote zilitoka sare ya bao 1-1.
Kipindi cha
pili kilianza kwa mwendo wa wastani huku ikionekana kama timu zikitegeana kwa
mashambulizi, walinzi wa Prison Laurian
Mpalile, Jumanne Elfadhil,Nurdin Chona na James Mwasote walikuwa na kazi ya
ziada ya kuokoa mashuti ya wachezaji wa Yanga ambao mara kadhaa walilikaribia eneo
la hatari na mipira ya kuokolewa.
Dakika ya 63
Mohamed Mkopi aliipatia Prison bao la pili lililotokana na faulo aliyofanyiwa
mchezaji wa Prison Juma Seif Kijiko na hivyo kuifanya Prison iongoze kwa bao
2-1.
Goli hilo
lilisababisha wapenzi na wanazi wa Yanga kuanza kukata tamaa ya ushindi kwa
siku hiyo huku wachezaji wa timu ya Prison wakionesha ari kubwa ya kuuwania
ushindi dhidi ya Yanga wakitamani kurejesha historia ya miaka 12 iliyopita mwaka 2003
ambapo Yanga ililala kwa bao 2-0.
Tafrani ya
kufungwa ilisababisha mshabiki mmoja maarufu wa Yanga Mama Yanga kuanguka chini
na kupoteza fahamu na kuchukuliwa na gari la wagonjwa kukimbizwa Hospitaliu ya
rufaa Mbeya huku mshabiki mkubwa wa Yanga maarufu kwa jina la Ali Yanga
akionekana kuhaha kila kona mithili ya mtu aliyechanganyikiwa akili.
Dakika
zilizidi kusonga huku Yanga ikionekana kukata tama ilhali timu ya Prison ikijionea
mwanga wa matumaini ya ushindi ndipo zikiwa zimesalia dakika 4 kabla ya kumalizika
mchezo mnamo dakika 86 mlinzi wa Prison James Mwasote aliunawa mpira eneo la
adhabu na hivyo refarii wa mchezo huo kutoa penati iliyopigwa na Simon Msuva na
kufunga goli.
Goli hilo
lilileta uhai kwa benchi la ufundi la Yanga lililokuwa chini ya Kocha Hans
Pluijm na kocha msaidizi Juma Mwambusi ambao kwa muda wote wa mchezo walikuwa
wanashindwa kukaa kwenye benchi wakihaha kila kona kuwapanga wachezaji wao
waliokuwa butu safu ya ushambuliaji.
Hadi
Kipyenga cha mwisho kinapulizwa Prison 2 Yanga 2.
Post a Comment