Ads (728x90)

Mwandishi wa MwanaSpoti Mwanahiba Richard anayedai kupigwa na Mwinyi Kazimoto


Mchezaji wa Simba anayedaiwa kumpiga mwandishi wa habari wa MwanaSpoti

Mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto amefikishwa kituo kikuu cha polisi mkoani Shinyanga, kwa tuhuma za kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la MwanaSpoti Mwanahiba Richard.

Kazimoto anayedaiwa kufanya kosa hilo kutokana na kudai kuwa mwandishi huyo aliwaandika vibaya kuwa wachezaji wa Simba waliocheza mechi ya Prisons na Mbeya City walikuwa chini ya kiwango na wanapaswa wachunguzwe kwa maana ya kuwa wamepewa rushwa.

Akizungumza juu ya tukio hilo kama alivyokuwa akizungumza na kituo kimoja cha redio usiku huu Mwanahiba alikuwa na haya ya kusema;

''Stori hiyo mie niliandika mwaka jana,..kuna siku alinipigia simu akaniuliza ni nani amekupa hiyo stori, nikamwambia siwezi kumwambia 
aliyenipa stori akaanza kunitukana kwenye simu,

Jana tulipokuwa uwanja wa kambarage wakati tunamfuata kocha akanifuata na kuniuliza wewe ndiye Mwanahiba nikamjibu ndiyo akasema unakumbuka niliwahi kukupigia simu nikamwambia ndio akasema mbona hujaniambia aliyekupa hiyo stori?

Nikamjibu mie sina mamlaka ya kukutajia aliyenipa hiyo stori nilishaipeleka gazetini na ikatumika akaniuliza sasa unaamua nini, nikamjibu mie sina la kuamua, akasema sasa yeye anaamua akaanza kunitukana na kunipiga...mie nikaamua kwenda polisi, hivyo ndivyo ilivyokuwa"...SAYZ MWANAHIBA


Post a Comment