Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Mbeya kwenye ukumbi wa Mkapa leo mchana |
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa Mariam Mtunguja alipokutana na wanahabari wa mkoa wa Mbeya leo mchana |
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano wa TAJATI Felix Mwakyembe akizungumza jambo mbele ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla kwenye ukumbi wa Mkapa leo mchana |
Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla kwenye ukumbi wa Mkapa leo mchana |
-Awataka
waandike habari za kweli zenye changamoto
-Asisitiza
hakuja Mbeya kufanya siasa
MKUU wa mkoa
wa Mbeya Amos Makalla ametoa somo kwa wanahabari akiwataka waibue habari za
kweli na zenye changamoto zitakazoisadia serikali huku akijitanabahisha mbele
yao kwamba amekuja mkoani Mbeya kwa ajili ya kufanya kazi na wala hakuja
kufanya siasa.
‘’Nataka
wanasiasa wajue kuwa mie sifanyi siasa bali nimekuja kufanya kazi, najua wazi
kuwa Jiji la Mbeya na halmashauri yake iko chini ya upinzani,wanasiasa wafanye
siasa zao mie ninafanya kazi,’’alisema
Alibainisha
kuwa kamwe hatahusisha utendaji wake na mambo ya siasa ingawa baadhi ya
wanasiasa wanadhani utendaji wake unashinikizwa na kasi za kisiasa,’’alifafanua.
‘’Mie ni
mtoto niliyekulia Baracks Police, baba yangu na mama yangu walikuwa ni askari
polisi, wote wameshatangulia mbele ya haki, Baba yangu aliniusia Nikipewa nifanye
kikweli kweli, na kiukweli ninapopewa kazi nafanya kazi kila nilipopewa
majukumu huwa natimiza wajibu wangu i am serious nimekuja kufanya kazi sio
siasa,’’alisisitiza.
Sanjari na
azma yake hiyo ya kufanya kazi pia amewataka wanahabari kushiriki katika kuibua
changamoto zilizopo ili ziweze kusukuma mbele maendeleo ya mkoa wa Mbeya katika
nyanja za kiuchumi na kijamii.
Akizungumza
katika kikao maalum na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mkapa, Makalla
alisema wanahabari ni sekta muhimu inayoweza kuisaidia serikali katika kuibua
mambo ya msingi ambayo yanaweza kuchukuliwa na kufanyiwa kazi na serikali.
‘’Tusaidiane
mnapoona mapungufu serikalini, andikeni hata habari zenye changamoto bali andikeni
habari zenye ukweli,’’alisema Makalla.
Aidha
Makalla ameelezea changamoto mbalimbali za utendaji zilizopo kwa watumishi wa
umma huku akiweka bayana tatizo la watumishi hewa ambalo limeisababishia hasara
serikali na kuwa amedhamiria kurejesha dhana ya utumishi bora kwa watumishi wa
umma.
Awali Mkuu
huyo wa Mkoa alipokea taarifa mbalimbali zenye changamoto kutoka kwa waandishi
wa habari kutokana na utendaji baina ya wanahabari na ofisi ya mkuu wa mkoa
ikiwa ni pamoja matatizo ya watendaji wa halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa
ugawaji viwanja holela katika maeneo ya wazi.
Post a Comment