Ads (728x90)



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiagiza kupunguzwa kwa gharama za upangaji wa soko la Mwanjelwa alipotembelea jana kufuatilia maagizo aliyoyatoa kwa watendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya



Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa alipotembelea soko jipya la Mwanjelwa jana.


MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla amekonga nyoyo za wafanyabiashara na wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuagiza kupunguza gharama za upangaji katika vizimba vya soko hilo jipya la Mwanjelwa kutoka Sh.500,000 hadi sh 350,000.

Maagizo hayo ameyatoa mara alipotembelea kwa mara ya pili soko hilo kwa nia ya kufuatilia maagizo aliyoyatoa katikati ya wiki sokoni hapo ikiwa ni pamoja na kutowapangisha wafanyabiashara kwenye eneo la dampo la takataka.

Huku akishangiliwa na wafanyabiashara wa soko hilo Makalla pia aliagiza vizimba vyote vilivyopo nje ya soko hilo kulipiwa sh. 1000 kwa siku sawa n ash. 30,000 kwa mwezi badala ya sh. 90,000 inayolipwa sasa.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara kufika sokoni hapo na kuomba vizimba na maduka na kutoa ofa ya mwezi mmoja wa Mei kutolipia kodi ili kutoa unafuu kwa wananchi na kuongeza wapangaji.

Post a Comment