Ads (728x90)



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amoss Makalla akiwa ndani ya jezi ya timu ya Mbeya City

Kapteni wa timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita Amos Gabriel Makalla ametua kwenye timu za soka zinazocheza Ligi Kuu zilizopo Jijini Mbeya,Prison na Mbeya City  na kuwataka viongozi wa timu hizo kumtumia vyema ili kuupa heshima mkoa wa Mbeya.

Makalla ambaye ndiye Mkuu wa mkoa wa Mbeya kwa sasa alipata kuiongoza timu ya bunge kwa mafanikio makubwa kwa kipindi chote cha  miaka 10 aliyekuwepo bungeni na kusema kuwa atatumia mbinu na  uzoefu wake katika medani ya soka kuhakikisha timu hizo zinafanya kwa mafanikio katika mechi zilizosalia.

‘’ Ee Mola wangu kwa niaba ya Wanambeya naziombea ushindi timu za mkoa wa Mbeya, Prison na Mbeya City ili ziweze kubaki ligi kuu, nawaomba wakazi wote wa mkoa wa Mbeya tushirikiane ili kuzipa sapoti timu zetu,’’alisema RC Makalla.
Mheshimiwa Makalla pia alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa timu ya Prison kumpatia jezi ya timu hiyo kwa kuwa yeye ni mlezi wa timu zote mbili za mkoa wa Mbeya.

‘’Mimi ni mlezi wa timu za madaraja yote mkoa wa Mbeya, naombeni ushirikiano wenu, Viongozi wa Prison naombeni jezi ya timu yenu,’’alisema Makalla.
Hivi karibuni viongozi wa timu ya Mbeya City walitumia fursa yao ya kukutana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na kumkabidhi jezi ya timu hiyo.


Post a Comment