Ads (728x90)


 Baadhi ya wazee na wananchi waliohudhuria ukumbi wa Mkapa kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla jana

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na wazee kwenye ukumbi wa Mkapa jana
 


Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa akizungumza wakati wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa MBEYA Amos Makalla jana
MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla ameunda kikosi kazi cha watu 14 kilichogawanyika katika makundi mawili ambacho kitapitia upya uhakiki wa majina ya watumishi hewa na kurejea kufanya uhakiki kati ya April 20 hadi 24.
Makalla aliagiza uhakiki huo kufanyika kati ya tarehe 25 hadi 29 ambapo awali alipata taarifa ongezeko la watumishi hewa 3 katika halmashauri ya Jiji la Mbeya na watumishi 7 kutoka halmashauri ya Mbeya.
Alisema katika uhakiki wa awali  Mkoa wa Mbeya na Songwe uligungulika kuwa na watumishi hewa 94 waliosababisha hasara ya sh milioni 457 na kuwa hadi sasa kuna jumla ya watumishi hewa 10 kati ya watumishi hewa saba ambapo Halmashauri ya Mbeya ina jumla ya watumishi 23 kutoka watumishi hewa 16 waliotajwa awali.
Makalla amewataka wafanyakazi wote kufika mbele ya kamati wakiwa na barua ya mwajiri, vitambulisho na Payroll ya mwezi Machi 2016 na kuiagiza kamati mara baada ya kufanya uhakiki watakaobainika na kesi za kujibu waburuzwe mahakamani na kutakiwa kurejesha fedha zote za serikali.


Post a Comment