Ads (728x90)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akiangalia ujenzi wa Meli za abiria bandari ya Itungi wilayani Kyela leo mchana

Sehemu ya Ufukwe wa Ziwa Nyasa Bandari ya Itungi wilayani Kyela


Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akioneshwa eneo la ujenzi wa meli bandari ya Itungi wilayani Kyela leo mchana



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla  amemwagiza mkandarasi kampuni ya Songioro Marine kukamilisha ujenzi wa meli 3 za Abiria ambazo zinajengwa na kampuni hiyo kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa mara baada ya kutembelea Bandari ya Itungi(Itungi Port) iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya ameridhishwa na muendelezo wa ujenzi wa meli hizo ambapo meli ya kwanza inatarajiwa kumalizika Agosti Mwaka huu.
Alisema Meli hiyo itakuwa na uwezo kubeba abiria 200 na tani 200 pamoja na magari 10-15.
‘’Meli ya pili yenye uwezo wa kubeba tani 1000 za mizigo ambapo meli ya tatu ambayo pia ina uwezo wa kubeba tani 1000 inatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2017,’’alisema Makalla.
Amefafanua kuwa kukamilika kwa meli hizo kutarahisisha usafiri kwa mikoa inayopakana na Ziwa Nyasa ambayo ni Mbeya(Kyela)Njombe(Ludewa)Ruvuma(Nyasa) na nchi jirani za Malawi na Msumbiji ambapo wananchi watanufaika kibiashara kati ya nchi hizo.
Aidha ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati na Wizara ya Ujenzi ili kuhakikisha barabara ya km 6 ya Itungi kuelekea Njiapanda Kiwira itajengwa kwa kiwango cha lami ili bandari hiyo ifikike kiurahisi.

Mheshimiwa Makalla pia amezitaka ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mbeya(RAS),DC na Menejimenti ya Bandari kuitangaza Bandari ya Itungi ili wananchi wazitambue fursa zilizopo ndani na nje ya nchi. 



Post a Comment