Ads (728x90)

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitembelea soko jipya la Mwanjelwa jana




Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na baadhi ya wafanyabiashara alipotembelea soko jipya la Mwanjelwa jana





Mkuu wa mkoa wa MBEYA Amos Makalla jana ametembelea soko jipya la Mwanjelwa na kutoa maagizo mazito baada ya kutoridhishwa na taarifa za uendeshaji wa soko hilo.

Katika ziara yake Makalla alibaini gharama kuba ya kodi ya upangaji ambayo inaonekana kutoendana kipato halisi cha wafanyabiashara na hivyo kuwaagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kukaa meza moja na wakopeshaji Benki ya CRDB ili kuangalia uwezekano wa kuwapunguzia kodi wafanyabiashara wa soko hilo.

Kadhalika amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU) ashirikiane na Ofisi ya Usalama wa Taifa kufanyia uchunguzi suala hilo ndani ya mwezi mmoja kuchunguza mchakato mzima wa ujenzi ulivyofanyika.

Post a Comment