Ads (728x90)


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iyunga

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla akimkabidhi vitanda kwa ajili ya mabweni ya wanafunzi yaliyoteketea kwa moto Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari Iyunga Steven Mwakajumilo

 
-RC Mbeya aokoa jahazi

-VETA yakubali kuwakopesha vitanda

Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambayo awali walidaiwa ‘kuramba’ zaidi ya Sh. milioni 50 kwa ajili ya harambee hewa ya kuchangia ujenzi wa mabweni, imekumbwa na fedheha baada ya kushindwa kukomboa vitanda 250 vyenye thamani ya sh. milioni 70.
Vitanda hivyo ni kwa ajili mabweni ya wanafunzi katika yaliyoungua moto katika shule ya sekondari Iyunga mwanzoni mwa mwaka huu ambapo uongozi wa Jiji la Mbeya ulitumia gharama kubwa kwa ajili ya kufanya harambee jijini Dar es salaam ambayo baadaye iliahirishwa.
Fedheha hiyo imewakumba watendaji wa Halmashauri wa Jiji baada ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla kuamua kuingia katika mabweni na kubaini kuwa wanafunzi wanalala chini kwa kukosa vitanda.
Vitanda 250 vilivyotengenezwa kwa ajili ya mabweni ya shule hiyo na Chuo cha VETA vilizuiliwa baada ya Halmashauri ya Jiji kushindwa kuvikomboa kwa gharama ya sh milioni 70 na kusababisha wanafunzi kulazimika kulala chini.
Mara baada ya kuwasili shuleni hapo Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye alipanga kuzungumza na wadau wa shule hiyo ili kutoa muongozo wa tahadhari kwa matukio ya majanga aliamua kutembelea kwenye mabweni na kukuta magodoro ya wanafunzi yakiwa yametandikwa chini.
Mkuu wa shule hiyo alimweleza Mheshimiwa Makalla sababu za wanafunzi kulala chini imetokana na Chuo cha VETA kuzuia vitanda ambavyo halmashauri ya Jiji la Mbeya bado haijavikomboa.
Kufuatia hali hiyo Mheshimiwa Makalla aliagizwa ndani ya saa moja vitanda hivyo viletwe shuleni hapo na kuitaka Halmashauri ya Jiji kulipa deni hilo kwa awamu ndani ya mwezi mmoja.
Aidha Mkuu wa mkoa pamoja na kuwaeleza wadau na viongozi wa shule hiyo kuhusu tahadhari ya majanga ya moto aliwataka wanafunzi kuwa walinzi wa matukio ya aina hiyo ili kuepusha madhara yanayoliingiza hasara Taifa.

Post a Comment