Ads (728x90)


Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Agosti 8, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na Waandishi wa Habari na kutoa taarifa za ujio wa Waziri Mkuu kwenye Ofisi za TAJATI leo asubuhi


Mheshimiwa Makalla akisalimiana na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za TAJATI leo asubuhi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ofisi za TAJATI leo asubuhi kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya Mariam Mtunguja
 

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI Christopher Nyenyembe (kushoto)akielezea maudhui ya chama hicho mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya leo asubuhi

Mwenyekiti wa TAJATI Taifa Ulimboka Mwakilili akimuonesha Mheshimiwa Makalla baadhi ya picha za kazi za wanatajati.


Waandishi wa habari wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Katibu Tawala Mariam Mtunguja walipotembelea Ofisi za TAJATI leo asubuhi.

 Mara nyingi huwa anakuwa nyuma ya kamera''Mratibu wa Habari na Mahusiano wa TAJATI Rashid Mkwinda alipata fursa ya kusalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla  alipotemebelea Ofisi za TAJATI leo asubuhi.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa anatarajiwa kuzindua Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) Agosti,8, 2016.
Akitoa taarifa hizo katika Ofisi za TAJATI leo asubuhi Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla alisema amefurahishwa na malengo ya chama hicho kwa kuwa kitachangia kuchochea Utalii na Uwekezaji nchini na kuwa uzinduzi wa chama hicho utafanywa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano.
‘’Tunamtarajia Waziri Mkuu Agosti 8, wakati wa maonesho ya Kilimo kanda ya Nyanda za Juu, moja ya kazi za mwanzo kuzifanya siku hiyo ni kuzindua Chama Cha Waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI)’’ alisema.
Mheshimiwa Makalla ambaye aliyetumia fursa hiyo kufahamiana kwa karibu na wanaTAJATI alisema kuwa chama hicho kina fursa ya kubwa ya kuibua na kutangaza Utalii na Uwekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuwataka kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara,kituo cha Uwekezaji(TIC), Wizara ya Maliasili na taasisi zake ikiwemo Bodi ya Utalii na TANAPA.
"Mkishirikiana vizuri na wizara hizo na taasisi zake na mkajitangaza nyinyi wenyewe na fursa tulizonazo nina uhakika utalii na uwekezaji utaongezeka nchini’’alifafanua.
Ili kujitangaza zaidi ndani na nje ya nchi Mheshimiwa Makalla aliwataka Wanatajati kufungua website(wavuti) ambayo itasaidia kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na TAJATI na manufaa yake kwa Taifa.
Aidha ameeleza kuwa moja ya shughuli alizopangiwa Waziri Mkuu mara atakapowasili mkoani Mbeya siku ya  tarehe 8/8/2016 ni kufanya uzinduzi rasmi wa  Chama hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TAJATI Taifa Ulimboka Mwakilili alisema kuwa chama hicho kimeshafanya ziara za ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuibua na kutangaza fursa za Utalii na Uwekezaji nchini hivyo ujio wa Waziri Mkuu utaibua hamasa kubwa katika kufuatilia fursa za Utalii na Uwekezaji nchini.
Wakati huo huo Mheshimiwa  Makalla amezitaka halmashauri za mikoa 7 ya nyanda za juu kusini , washiriki wa maonesho ya Nane nane, wananchi na wadau mbalimbali kuhakikisha maonesho ya mwaka huu yanakuwa ya dira na taswura ya kuigwa  kwa maonesho ya kanda zingine.
Akizungumza kwenye kikao cha mwisho cha maandalizi ya maonesho hayo ambayo yanajumuisha mikoa 7 ya Mbeya,Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma,Rukwa na Katavi, Mheshimiwa Makalla alisema maonesho hayo yatazinduliwa na Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na kufungwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa mikoa hii ya Nyanda za Juu Kusini ndiyo dira ya Kilimo na chakula kwa mikoa mingine nchini hivyo anatarajia maonesho hayo yawe ya mfano kwa kanda zingine zenye maonesho ya aina hiyo mwaka huu.

Post a Comment