Ads (728x90)





Awali ilidaiwa kuwa eneo lenye madini ghali na adimu duniani ya chuma kisichopata kutu aina ya Niobium na madini mengine ya Phosphate na Phlogopite yalihifadhiwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere eneo la Songwe nje kidogo ya Jiji la Mbeya kwa kujengwa gereza.
Ilielezwa kuwa lengo la Mwalimu kujenga gereza hilo eneo la Songwe lilikuwa na dhamira ya kuitunza hazina hiyo ili hatimaye ije kuwanufaisha watanzania katika miaka ijayo.
Moja kati ya madini hayo aina ya Niobium ambayo yanayotumika kutengenezea ndege na kompyuta yanachimbwa Bara Amerika ambapo kwa kuwepo mgodi huo mkoani Mbeya itakuwa ni mgodi wa kwanza kwa bara la Afrika na wa nne duniani utachangia kuinua uchumi wa Taifa.
Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla alifanya ziara kwenye eneo la machimbo ya mgodi huo na kukutana na Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited Derick ambaye alieleza kuwa utafiti wa machimbo hayo umefanyika kwa miaka mitano.
Alisema kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 ambao utasaidia kuonbgeza ajira kwa watanzania wapatao 500 na uzalishaji wake utaanza mapema mwaka 2018.
Mapema mwaka 2009 kulikuwa na mvutano wa eneo hilo ambalo linamilikiwa na gereza la mahabusu la Songwe juu ya uhalali wa umiliki kati ya makapuni mawili ya kigeni ambayo yalikuwa yakihitaji kuchimba madini eneo hilo.

Post a Comment