Awali
ilidaiwa kuwa eneo lenye madini ghali na adimu duniani ya chuma kisichopata
kutu aina ya Niobium na madini mengine ya Phosphate na Phlogopite yalihifadhiwa
na Hayati Mwalimu Julius Nyerere eneo la Songwe nje kidogo ya Jiji la Mbeya kwa
kujengwa gereza.
Ilielezwa
kuwa lengo la Mwalimu kujenga gereza hilo eneo la Songwe lilikuwa na dhamira ya
kuitunza hazina hiyo ili hatimaye ije kuwanufaisha watanzania katika miaka
ijayo.
Moja
kati ya madini hayo aina ya Niobium ambayo yanayotumika kutengenezea ndege na
kompyuta yanachimbwa Bara Amerika ambapo kwa kuwepo mgodi huo mkoani Mbeya
itakuwa ni mgodi wa kwanza kwa bara la Afrika na wa nne duniani utachangia
kuinua uchumi wa Taifa.
Hivi
karibuni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla alifanya ziara kwenye eneo la
machimbo ya mgodi huo na kukutana na Mkurugenzi wa kampuni ya Pandahil limited
Derick ambaye alieleza kuwa utafiti wa machimbo hayo umefanyika kwa miaka
mitano.
Alisema
kampuni hiyo itawekeza zaidi ya shilingi bilioni 500 ambao utasaidia kuonbgeza
ajira kwa watanzania wapatao 500 na uzalishaji wake utaanza mapema mwaka 2018.
Mapema
mwaka 2009 kulikuwa na mvutano wa eneo hilo ambalo linamilikiwa na gereza la
mahabusu la Songwe juu ya uhalali wa umiliki kati ya makapuni mawili ya kigeni
ambayo yalikuwa yakihitaji kuchimba madini eneo hilo.
Post a Comment