|
Mtoto Said(9) mkazi wa Suluti wilaya ya Namtumbo akiandaa chakula cha mchana |
|
Maandalizi ya ugali kwa ajili ya chakula cha mchana yanayofanywa na mtoto Said mkazi wa Suluti wilaya ya Namtumbo |
|
Ugali kwa dagaa chakula cha mchana |
|
Mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Said mkazi wa Suluti wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma amekutwa na kamera yetu wakati wa mchana akiandaa chakula kwa ajili ya mlo wa mchana. |
|
Said ambaye anasoma darasa la tatu amedai kuwa wazazi wake wako kwenye vibarua ili kujiongezea kipato kutokana na hali ngumu ya kiuchumi waliyonayo.
Alisema baba yake hufanya vibarua vya kulima mashamba ya watu na yeye kujipatia ujira mdogo unaowawezesha kupata chakula ambapo mama yake naye anafanya vibarua kwa ajili ya kusaidia shughuli za ujenzi na kuambulia senti kidogo zinazowasaidia kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani.
''Naandaa chakula ili nimpelekee mama kibaruani kwake, yeye anafanya kibarua cha kusaidia mafundi wanaojenga, baba analima vibarua huko mashambani'' anasema Said na kuongeza kuwa kila siku analazimika kutorudia shule mchana ili amudu kufanya shughuli za nyumbani na kupika chakula kumpelekea mama yake.
Post a Comment