Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Christopher Kilungu |
Minazi zao ambalo Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo inataka kulifanya kuwa ni zao la biashara |
HALMASHAURI ya wilaya ya Namtumbo imetenga bajeti ya Sh
milioni 10 kwa msimu wa kilimo wa
2016-17 ili kuimarisha zao la Korosho na minazi liweze kuongeza tija kwa
wakulima na kipato kwa Halmashauri ya wilaya hiyo.
Mazao ya Minazi na Korosho ambayo yamezoeleka kulimwa katika
mikoa ya Pwani yanatarajiwa kuongeza pato la Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo
baada ya kuonekana uwezekano mkubwa wa kustawi katika maeneo ya Kata za
Magazini,Lusewa,Likuyuseka na Kijiji cha Mandepwende.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
Christopher Kilungu alisema kuwa mkakati huo ni kwa ajili ya kuongeza uwekezaji
katika mazao ya biashara yenye uwezekano mkubwa wa kustawi wilayani humo.
Alisema Halmashauri katika bajeti yake ya mwaka 2016/17
imetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa mbegu na miche bora ya mazao ya biashara
ili kuwagawia wakulima kwa nia ya kuongeza uzalishaji wa mazao hayo na hatimaye
kuongeza kipato cha mkulima mmoja mmoja na kwa Halmashauri.
Kitundu alisema jumla ya miche 5000 ya minazi ambayo
itanunuliwa mkoani Mtwara itaanza kugaiwa kwa wakulima waanze kuzalisha zao
hilo ili kuepuka kufuata nazi katika mikoa ya Pwani jambo ambalo limekuwa ni
gharama kubwa kwa wafanyabiashara na kulifanya zao hilo kuuzwa kwa bei ya juu.
‘’Kwa utafiti wetu zao hili linastawi zaidi katika ukanda wa
kusini maeneo ya Mchomoro,Rwinga, Lusewa,Magazini, Likuyu na Msisima,tumepanga
kutumia shilingi milioni 5 kwa ajili
kununua miche kutoka Mtwaram’’alisema Kitundu.
Sanjari na zao la Minazi Kitundu alisema Halmashauri pia
imepanga kutumia sh. Milioni 5 kwa ajili ya kununua miche ya zao la Korosho
ambalo limeonekana kuwa na tija kwa wakulima kwa kipindi hiki.
Mazao mengi ya biashara ambayo alisema yanaweza kuibua
uwekezaji katika sekta ya kilimo ni pamoja na
Kahawa,Soya,Tangawizi,Mpunga,Choroko, Mbaazi na Ufuta ambapo baadhi ya mazao
kama vile Soya limeshapata mnunuzi kampuni ya Silverland ya mkoa wa Iringa
ambaye ameahidi kununua tani 9,000 hadi 11,000 kwa bei ya sh.1,000 badala ya
sh.750 iliyokuwa ikiuzwa msimu uliopita.
Post a Comment