Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima akisikiliza kero kutoka kwa mmoja wa wananchi wa mji wa Namtumbo alipozungumza na wananchi mwishoni mwa wiki. |
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima akisisitiza jambo mbele ya wananchi wa mji wa Namtumbo |
Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Luckiness Amlima akizungumza na wakazi wa mji wa Namtumbo |
MKUU wa wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Luckiness Amlima
amewaonya wanaume wa wilayani humo kuacha kuoa wake wengi ambao huwageuza kama matrekta kwa ajili ya shughuli za kilimo
mashambani.
Kadhalika Mkuu huyo amewataka wanawake kwa upande wao
kutumia mbinu mbadala kwa ajili ya kulinda ndoa zao ili wanaume wasishawishike
kuwaolea wanawake wengine.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliozihusisha kata
mbili za Namtumbo na Rwinga na vijiji vyake saba Amlima alisema ipo desturi kwa
wanaume wa wilaya hiyo kuwatumia wanawake kama nyenzo ya kuwatumikia wanaume
katika shughuli za uzalishaji mali.
‘’Nyie wanaume wa Namtumbo punguzeni kuoa oa na kuwafanya
wanawake kama matrekta ya kulimia, hali hiyo inachangia kupunguza uzalishaji wa
chakula, maana nguvu ya wanawake pekee haitoshi kutumika kuzalisha chakula
mashambani,na nyie akina mama wenzangu mjirekebishe,mnashindwa kuzitunza ndoa
zenu ndio maana wanaume hawatosheki wanawaolea wanawake wengine,’’alisema
Amlima.
Alisema mbali na wanawake pekee kutumika katika uzalishaji
wa chakula mashambani, wakati wa mavuno chakula hicho hicho kinachozalishwa na
mwanamke kinauzwa na mwanaume ambaye kutwa hushinda kucheza bao na kuongeza mke
mwingine hali ambayo inachangia kuwepo kwa unyanyasaji na dhidi ya mwanamke na
hata kukosekana kwa chakula cha akiba katika kaya.
‘’Nyie ni watani zangu nitawaeleza ukweli kama nawakosea
naomba mnisamehe lakini napaswa kusema ukweli juu ya vitendo vya unyanyasaji
wanavyofanyiwa wanawake wenzangu, mimi kama mwanamke mwenzenu najisikia
uchungu,’’alisisitiza huku kauli yake ikisindikizwa kwa vigelegele kutoka kwa
akina mama waliohudhuria mkutano huo.
Aidha alisema kuwa kipindi cha mavuno wananchi
wanamaliza chakula chote ghalani kwa
ajili ya ngoma, vigodoro na unyago kiasi
cha kukosa chakula cha akiba na mbegu hali ambayo inaweza kusababisha kuibuka kwa
baa la njaa.
‘’Tukipunguza mambo ya vigodoro na unyago wakati wa
kiangazi, hatutafikwa na njaa wakati wa masika, tujitahidi kuhifadhi chakula na
kupunguza ngoma na unyago,’’alifafanua Mkuu huyo wa wilaya ambaye huo umekuwa
mkutano wake wa kwanza hadharani tangu ateuliwe na Rais kushika wadhifa huo
Julai mwaka huu.
Katika hatua nyingine Amlima amesema kuwa wakazi wa mji huo
ambao asilimia kubwa ni waislamu wanapaswa kuwahimiza watoto wao kujifunza
imani za kiroho kwa kuwapeleka Madrasa na katika shule za kidunia ili wamjue
Mungu na wajue mambo ya dunia na hatimaye waweze kuishi katika maadili mema
yanayompendeza Mungu hapa duniani na baada ya kuondoka duniani.
austine88
ReplyDeletelink austine88
link alternatif austine88
Bandar online slot dan togel
agen slot terlengkap
slot gacor
situs judi online
bandar togel
slot online terbaik
agen slot dan togel
situs togel dan slot
togel singapore
slot online terpercaya
agen slot
Pragmatic Play
Deposit pulsa
Deposit pulsa
livegames casino