Washitakiwa wa kesi ya kuchoma Kor an tukufu wakiingia katika mahakama ya hakimu mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kusomewa mashtaka ya kosa linalowakabili |
Washitakiwa wa kosa la kuchoma Kor ani wakiwa kizimbani ndani ya Mahakama ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma |
Baadhi ya waumini wa Kiislamu wakiwa katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uchomaji wa Kor an |
Taharuki imeibuka katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa
Wilaya ya Namtumbo baada ya mshitakiwa namba moja kati ya washitakiwa sita wa
kesi ya jinai namba 48 ya mwaka 2016 kuanguka kizimbani na hivyo kulazimika Hakimu wa Mahakama hiyo Majinge
Kusaga kuahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21.
Hali iliyoibua taharuki mahakamani hapo imetokana na mshitakiwa huyo Rashid Ausi(75) ambaye ndiye
mshitakiwa nambari moja mara baada ya kupandishwa kizimbani alionesha dalili za
kuishiwa nguvu na kunyong’onyea huku akijitahidi kunyoosha mkono wake ili
aruhusiwe kuzungumza chochote.
Mara baada ya Hakimu kumruhusu kusema akazungumza kwa taabu
maneno mawili ‘NATAKA KULALA’ kama vile
hakusikia vyema alichosema mshitakiwa huyo alimtaka mshitakiwa kurudia tena
kueleza tatizo lake mara ya pili, kabla hajajibu kwa ufasaha alichohitaji mshitakiwa huyo alianguka chini na kulala
kizimbani na baadaye kubebwa na kulazwa pembeni kabla ya kusindikizwa Hospitali
ya wilaya ya Namtumbo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Maneno yake yaliyosikika kwa uchache kutoka kinywani mwake
yalikuwa ni kwamba anajisikia tumbo linamuuma na hata walipotakiwa baadhi ya
jamaa walioambatana naye wamsindikize chooni, mshitakiwa huyo alilala pembeni
ya benchi lililopo mahakamani humo ambapo wakati huo huo Hakimu aliomba
kuahirisha kesi hiyo kwa dakika 10 ambapo aliwataka jamaa wa mshitakiwa
kumpeleka hospitali mshitakiwa huyo.
Wakati mshtakiwa huyo akipelekwa hospitalini Hakimu Kusaga
alitamka kuiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21 ambapo upande wa Mashtaka
utawaleta mashahidi wa kosa hilo linalowahusu washitakiwa 6 ambao wanadaiwa
kuteketeza kwa moto vitabu vya dini ya Kiislamu (Koran) kutokana na shinikizo la imani za ushirikina.
Awali washitakiwa 6 wamefikishwa mahakamani hapo
wakituhumiwa kwa kosa la kuchoma Kor ani Tukufu,Kitabu kinachotumiwa na waumini
wa dini ya Kiislamu wakishtakiwa kwa kosa la kuharibu mali na kumuita mtu
mchawi.
Tukio hilo linadaiwa kutokea katika kijiji cha Ngwinde Kata
ya Litola wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo washitakiwa hao Rashid
Ausi(75)Shazir Rashid(31)Rashid Nchimbi(35)Abdalla Nchimbi(56)Kanuti
Nchimbi(53) NA Juma Ndembo(36) wanakabiliwa na mashtaka hayo.
Eneo la Mahakama ya wilaya ya Namtumbo lilihudhuriwa na
umati wa waumini wa dini ya kiislamu hali ambayo haijawahi kutokea katika
wakati mwingine na hivyo kuibua zaidi taharuki miongoni mwa watu waliokusanyika
mahakamani hapo kusikiliza kesi zingine.
Post a Comment