Mmoja wa washitakiwa akiwa ameanguka chini mahakamani kabla ya kuahirishwa kesi kwa mara ya kwanza, kesi inayowahusu imamu na mganga wa kienyeji wakishtakiwa kwa uchomaji wa Koran Tukufu |
Baadhi ya waumini wa Kiislamu wakiwa wamekusanyika katika mahakama ya wilaya Namtumbo kusikiliza kesi kabla haijaahirishwa wiki iliyopita, kesi hiyo itaanza kusikilizwa kesho Disemba Mosi |
Waumini wa Kiislamu wakisoma dua kumuomba Mwenyezi Mungu kufuatia kitendo cha Uchomaji Koran kilichodaiwa kufanywa na watu kwa aimani ya ushirikina |
Na Mwandishi Wetu, Namtumbo
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya
Namtumbo mkoani Ruvuma kesho inatarajia kuanza kusikiliza kesi inayowakabili waumini
sita wa dini hiyo wanaokabiliwa na kesi ya uchomaji wa Kor an Tukufu baada ya kuahirishwa siku 10 zilizopita kwa madai kuwa
mshitakiwa namba mbili Shazir Rashid (31) kuelezwa mahakamani hapo kuwa ameugua
ghafla ugonjwa wa kifafa.
Kesi hiyo ya jinai namba 48 iliahirishwa mara ya kwanza
Novemba 11, 2016, baada ya mshitakiwa namba moja Rashid Ausi(75) kuanguka
kizimbani kwa kile kilichoelezwa kuwa mshitakiwa huyo aliugua ghafla maradhi ya
tumbo.
Madai ya mshitakiwa wa pili wa kesi hiyo kukumbwa na ugonjwa
wa kifafa ilimsababisha Hakimu Mfawidhi
wa Mahakama hiyo Majinge Kusaga kuahirisha tena kesi hiyo hadi jana ambapo pia imeahirishwa tena
hadi Disemba Mosi baada ya mshitakiwa mwingine kushindwa kufika mahakamani kwa
madai ya kuugua ugonjwa wa kifafa.
Mara baada ya washitakiwa wote sita kuitwa mahakamani kwa
ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo orodha ya washitakiwa haikutimia
badala ya washitakiwa sita waliopaswa kupanda kizimbani walionekana washitakiwa
watano ndipo hakimu Majinge alitaka kujua alipo mshitakiwa namba mbili wa kesi
hiyo.
Hakimu Majinge alimuita mdhamini wa mshitakiwa huyo Cladius
Fungo ambaye aliithibitishia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa namba mbili Shazir
Rashid anaumwa ameanguka ugonjwa wa kifafa huko kijijini.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Majinge alilazimika kuahirisha
kesi hiyo hadi Disemba Mosi ambapo kesi hiyo italetwa tena mahakamani kwa ajili
ya kuanza kutolewa ushahidi.
Katika hatua nyingine kundi kubwa la waumini wa dini ya
Kiislamu ambao walihudhuria mahakamani hapo waliendelea kusimama wakionesha
dalili za kupata maelezo zaidi ya kuahirishwa kwa kesi hiyom ndipo mmoja wa
maaskari alitoa ufafanuzi na kuwaeleza waumini hao kesi hiyo imeshindwa
kusikilizwa kutokana na mshitakiwa namba mbili kushindwa kufika mahakamani kwa
maelezo kuwa anaumwa.
Mara baada ya waumini wa dini hiyo kuondoka mahakamani hapo
walirejea katika msikiti mkuu wa wilaya ambapo kwa pamoja waliamua kufanya dua
kwa kile walichoeleza kuwa wanaomba usaidizi kwa Mwenyezi Mungu juu ya tukio
zima la uchomaji wa Koran lilivyofanyika.
Kaimu Shekhe wa wilaya hiyo Ahmad Banda alisema kuwa
wanamtumia jukumu hilo Mwenyezi Mungu ili kuepusha laana ambayo anaweza
kuishusha kuathiri watu wasio na hatia.
Shekhe Banda alisema kitendo kilichofanyika cha uchomaji Kor
an kinaweza kuleta balaa kwa jamii, ili laana isiwakute wasiohusika na kwamba
wameamua kufanya dua na kuwa wataendelea
kufanya dua kila Ijumaa, kumlilia Mwenyezi Mungu.
Post a Comment