Ads (728x90)




Google Chrome

Kwa nini utumie Google Chrome?

Google Chrome ni kivinjari wavuti kinachoendesha kurasa na programu za wavuti kwa kasi ya umeme. Soma kuhusu ni kwa nini tuliunda kivinjari.
  1. Kasi

Kasi: Huanza haraka, na hupakia kurasa za wavuti kwa kasi

    • Ni nyepesi kuianzisha kutoka kwenye eneo-kazi lako
    • Hupakia kurasa za wavuti mara moja
    • Huendesha programu za wavuti haraka zaidi

2.      Urahisi: Imeunda kwa ajili ya uthabati na urahisi wa matumizi

    • Tafuta na uabiri hadi kurasa za wavuti kutoka kwenye kisanduku kimoja
    • Panga na unadhifishe vichupo jinsi unavyotaka — haraka na kwa urahisi
    • Fika kwenye tovuti uzipendazo kwa kubofya mara moja tu, kutoka kwenye vijipicha vya tovuti unazozitembelea zaidi kwenye ukurasa wa Kichupo Kipya
  1. Mandhari

Mtindo: Mandhari ya kusisimua kivinjari chako

Tazama Onyesho la YouTube kuhusu Mandhari ya Google Chrome kutoka kwa Wasanii.
Kwa maelezo zaidi kuhusu vipengele vya Google Chrome, tazama Kituo cha Msaada cha Google Chrome.
Kwa masasisho mapya zaidi, soma Blogu ya Google Chrome.
©2011 Google - Nyumbani Google - Kuhusu Google - Msaada - Sera ya faragha - Wasanidi tovuti - Programu huria


Google Chrome

Mtazamo mpya kwa kivinjari
Hapa Google, huwa tunatumia muda wetu mwingi tukifanya kazi ndani ya kivinjari. Sisi hufanya utafutaji, kupiga gumzo, kutuma barua pepe na kushirikiana katika kivinjari. Na kama nyinyi wote, katika muda wetu wa ziada, huwa tunanunua vitu, kwenda benki, kusoma habari na kuwasiliana na marafiki - yote kupitia kivinjari. Watu wanatumia muda zaidi na zaidi kwenye wavuti, na wanafanya mambo ambayo hayakuwahi kudhaniwa wavuti ulipojitokeza kama miaka 15 iliyopita.
Kwa sababu sisi hutumia muda mwingi sana kwenye wavuti, tulianza kuwaza sana kuhusu kivinjari ambacho kingeweza kuwepo ikiwa tungeanza kutoka mwanzo na kikiunda kwa kutumia sehemu bora zaidi zilizokuwepo. Tulitambua kuwa wavuti ulikuwa umebadilika kutoka sana sana kurasa rahisi za maandishi hadi programu anuwai na wasilianifu na kuwa tulihitaki kukifikiria kivinjari upya kabisa. Tulichohitaji kilikuwa sio kivinjari tu, bali jukwaa la kisasa la kurasa za wavuti na programu, na hicho ndicho tulipanga kuunda.
Kijuu juu, tuliunda dirisha la kivinjari la kisasa na rahisi. Kwa watu wengi, sio kivinjari kilicho cha umuhimu. Ni zana tu ya kuendesha vitu vilivyo na umuhimi - kurasa, tovuti na programu zinazounda wavuti. Kama ukurasa wa nyumbani wa Google, Google chrome ni safi na nyepesi. Inakuondokea na kukufikisha unakotaka kwenda.
Chini ya chadarua, tuliweza kuunda msingi wa kivinjari kinachoendesha programu wavuti za kisasa kwa njia bora zaidi. Kwa kuweka kila kichupo katika "sanduku" pweke, tuliweza kuzia kichupo kimoja kuzima kingine na kutoa ulinzi dhidi ya tovuti mbaya. Tumeboresha kasi na mawasiliano katika sehemu zote. Pia tuliunda v8, injini ya JavaScript yenye uwezo zaidi, kuendesha kizazi kijacho cha programu za wavuti ambazo haziwezekani na vivinjari vya sasa.
Huu ndio mwanzo tu - mambo bado kwenye Google Chrome. Tumezindua toleo hili la beta kwa ajili ya Windows ili kuanzisha majadiliano mapana na tuwese kusikia kutoka kwako haraka iwezekanavyo. Tunajitahidi kuunda matoleo ya Mac na Linux pia, na tutaendelea kuifanya iwe nyepesi na yenye nguvu hata zaidi.
Tunawia deni kubwa kwa miradi mingi ya programu huria, na tumejitolea kuendelea katika njia yao. Tumetumia sehemu za WebKit ya Apple na Firefox ya Mozilla, na nyinginezo - na katika moyo huo, tunafanya hati fumbo yetu iwe huria pia. Tunatazamia kushirikiana na jumuiya yote ili kusaidia kuusukuma wavuti mbele.
Wavuti huimarika kwa chaguo na uvumbuzi zaidi. Google Chrome ni chaguo lingine, na tunatumai kuwa itachangia katika kuboresha wavuti hata zaidi.
Haya basi kutoka kwetu. Uhondo wa Google Chrome ni uijaribu mwenyewe.
©2011 Google - Nyumbani Google - Kuhusu Google - Msaada

Post a Comment