Ads (728x90)



MADIWANI 24 wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wanafanya ziara ya siku nne wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya kwa nia ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo,utoaji huduma za kiafya CHF,Masjala ya ardhi na mafanikio ya ukusanyaji wa kodi kwa ngazi za vijiji, mitaa na wilaya.

Akizungumza kwa njia ya simu juu ya ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Namtumbo Bw. Mussa Zungiza(pichani juu) alisema kuwa ziara hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Bw. Stephan Nana ambayo italenga kujifunza mafanikio mbalimbali ambayo halmashauri ya wilaya Mbozi imeyapata kutokana na kujali utawala bora kati ya wananchi na watendaji wa serikali.

Bw. Zungiza alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina fursa nyingi za kiuchumi zikiwemo zile zitokanazo na mazao ya biashara na chakula kama vile Tumbaku,Korosho,Ufuta, Alizeti na mazao ya chakula ambayo ni mahindi na mpunga ambayo iwapo wananchi wakiyatumia vyema wanaweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmaashauri ya Wilaya ya Mbozi Levison Chillewa

''Wilaya hizi zinafanana kwa kila hali kuanzia mazao yanayolimwa. jiografia yake... ni muhimu kujua mbinu mbadala za uzoefu ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi ndani ya halmashauri yetu,''alisema.
 ''Tumezingatia mafanikio ya Mbozi katika maeneo mengi 
..kama vile ukusanyaji kodi kwa ngazi za vijiji, kata na wilaya, uundwaji wa miji midogo, hati miliki za kimila ambazo wananchi wanakopesheka kutokana na ardhi yao ya asili,''alisema Bw. Zungiza.

Alifafanua kuwa Wilaya ya Mbozi imefanikiwa katika usimamizi wa miradi kutoka ngazi za kata na vijiji jambo ambalo linaonesha kuna ushirikishwaji mkubwa baina ya watendaji wa serikali na wananchi.

Bw. Zungiza alisema kuwa ziara hiyo inaanza leo na kukamilika Januari 20 ambapo ambapo pia madiwani hao watapata fursa ya kutembelea wilaya ya Njombe iliyoko mkoani Iringa ambakoina mandhari na jiografia inayoshabihiana na wilaya ya Namtumbo.
 ''Wilaya hizi zinafanana kwa kila hali kuanzia mazao yanayolimwa. jiografia yake... ni muhimu kujua mbinu mbadala za uzoefu ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi ndani ya halmashauri yetu,''alisema.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw.Levison Chilewa alisema kuwa, mafanikio ya Halmashauri hiyo yanatokana na ushirikishwaji uliopo baina ya watendaji wa serikali na wananchi ambapo hamasa kubwa imetokana na wananchi kukubali kuhudhuria mikutano ya vijiji na kata na kwamba viongozi wa serikali wamehimizwa kuwa na utaratibu wa usomaji wa mapato na matumizi kwa wananchi.

Post a Comment