Ads (728x90)


Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Dkt.Wilbroad Slaa anatarajia kutua Jijini Mbeya Januari 10 kwa ziara ya kuhamasisha chama mkoani humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa CHADEMA mkoani Mbeya Eddo Makatta anasema kuwa Dkt. Slaa ataingia Jijini Mbeya na kufanya mikutano ya ndani kisha mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali ya wazi.
Makatta alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho kukutana na wapiga kura wake kwa nia ya ,kuwazindua juu ya mambo mbalimbali ya hujuma na ufisadi dhidi ya wananchi unaofanywa viongozi waliopo madarakani.
Alisema kuwa ziara ya Dkt. Slaa inakuja wakati kukiwa na mijadala na midahalo mbalimbali inayoendelea juu ya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.



Post a Comment