Ads (728x90)



CCM  imemtangaza mgombea Ubunge katika Jimbo la Arumeru Siyoi Sumari aliyepata kura 761 dhidi ya kura 361 alizopata mpinzani wake wa karibu Bw.William Sarakikya.
Kwa hutua hiyo Bw.Sumari ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Bw. Jeremiah Sumari ndiye atakayepeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi hiyo dhidi ya vyama vya vingine hususani CHADEMA.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa uchaguzi huo Bw. Pius Msekwa ni kwamba uchaguzi huo umerudiwa baada ya uchaguzi wa awali kumkosa mshindi kutokana na wagombea kupata kura chini ya asilimia 50.
Katika uchaguzi wa awali Sumari alipata kura 316 na Sarakikya alipata kura 259.
Uchaguzi huo umefaanyika baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Bw.Jeremiah Sumari aliyefariki Januari 19 mwaka huu.

Post a Comment