Wakiwa wamelowa kwa mvua kutokana na umbali wa shule na kunyeshewa hujikuta wakiwa wamejikunyata kwa baridi.
MKASA WA MAISHA
Ni majira ya saa 11 00 alfajiri mama anamuamsha mwanaye aliyepaswa kuwa shule ya msingi kwa ajili ya kuwahi kufanya kibarua cha kuchunga ng'ombe katika pori lililopo umbali wapata kilomita 20 kutoka nyumbani anakoishi.
Huko ndiko maeneo stahiki kwa ajili ya malisho ya Ng'ombe angalau warudipo jioni huwa na uwezo wa kutoa lita kadhaa za maziwa na yeye kupata lita moja ya kupeleka nyumbani ambako mama yake huuza na kupata angalau mlo wa siku hiyo.
Nimelazimika kuandika makala haya bila kutaja kijiji ili kuweka uthamani wa stori hii na kuzuia watu kuimiliki bila idhini ya mtafutaji wa stori.
Mtoto huyu (EZEKIEL) sio jina kamili amezoea kuishi kwa utaratibu huo tangu aanze kujitambua kwa umri mdogo alionao huku mama yake mzazi fukara asiye na uwezo akimfanya ni sawa na baba mlezi wa nyumba yao chakavu katika kijiji hicho.
Maisha ya familia hii hugubikwa na ukiwa hususani nyakati za jioni na usiku, huku kibanda waishicho cha mbavu za mbwa kikishindwa kuzuia mvua, baridi nyakati za usiku na jua wakati wa mchana.
Umbali mrefu kutoka katika kijiji aishicho mtoto huyu kuna kijiji kingine ambako kuna shule ya msingi, huko nako watoto hulazimika kusafiri umbali mrefu kufika shuleni na hupata adha nyakati za masika kwa kuchelewa kufika shuleni ambapo mvua kubwa inayonyesha hutenganisha makazi yao.
Kati ya kijiji na shule kuna bonde linalojaa maji nyakati za masika mara nyingine watoto huchelewa kufika shuleni kutokana na mfereji kukatisha mawasiliano, ambapo wapita njia na wasamaria wema hujitahidi kuwavusha.
Umbali wa kutoka shuleni hadi nyumbani husababisha watoto kunyeshewa na mvua na wanapofika shuleni huwa wametota na mvua kiasi cha kushindwa kuzingatia vyema masomo.
Kwa upande wake mzazi wa mtoto Ezekekiel ambaye hujikunja pembeni ya zizi la ng'ombe hutafakari mengi juu ya maisha yake ya kijijini na mara nyingine hujikuta akiwaza mengi na kuona namna ambavyo dunia imemuelemea bila mafanikio yoyote na kutamani walau ardhi ipasuke na kumfunika. |
dah inasikitisha jamani hata sijui naweza kutoa mchango gani ila kwa staili hiyo hawawezi kufanikiwa katika masomo yao maana ni mazingira magumu sana kwa kweli
ReplyDelete