PRISON ya Mbeya leo jioni imekataa kuipaisha Simba ya Dar es salaam kwa kutoka nayo suluhu ya 0-0 na kuifanya ibaki nafasi ya nne nyuma ya timu ya Mbeya City kwa kubaki na Pointi 36 huku Prison ikiwa na point 22 ikiwa nafasi ya 10.
Azam ndiyo inayongoza Ligi hiyo ikiwa na jumla ya pointi 40 ikifuatiwa na Mbeya City yenye pointi 39 Yanga yenye pointi 38 inashikilia nafasi ya tatu ilhali Simba ikiwa na pointi 36 ikishikilia nafasi ya Nne.
Prison yenye Pointi 18 inaendelea kubaki nafasi ya 10.
Mchezo huo uliokuwa ukichezwa kwa kupaniana ulianza kwa kasi chini ya Mwamuzi Isihaka Shirikisho kutoka Jijini Tanga ulikuwa mgumu kwa kila upande kutokana na kila timu kulinda lango lake lisishambuliwe na mwenzie.
Dakika ya 32 ya kipindi cha kwanza mchezaji Jumanne Elfadhil wa Prison alizawadiwa kadi ya njano kwa kumchezea mchezo mbaya Hamisi Tambwe wa Simba ambaye kwa mchezo huo alioenekana kudhibitiwa sana na Nurdin Chona.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka suluhu 0-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo timu ya Prison iliwaingiza Bryton Mponzi aliyeingia badala ya Peter Michael, Jimmy Shoji aliyeingia badala ya Omega Seme.
Simba ilifanya mabadiliko ambapo mchezaji Awadhi Juma aliingia badala ya Ramadhan Singano na Haruna Chanongo aliingia badala ya Betram Mwombeki.
Hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuleta mabadiliko yoyote kwa kila timu zaidi ya kila timu kuanza kutoonesha uchezaji wake makini na kuanza mchezo wa piga nikupige.
Aidha katika dakika ya 30 ya mchezo wachezaji Nurdin Chona wa Prison na Hamis Tambwe wa Simba waligongana na kutoana ngeu huku Nurdin akipasuka eneo la jicho na kuvuja damu na Hamis Tambwe akitobolewa kichwani na kupatiwa matibabu kisha wachezaji wote kuendelea na mchezo wakiwa wamefungwa bandeji huku wakivuja damu.
Hadi Kipyenga cha mwamuzi Shirikisho kutoka Jijini Tanga kinapulizwa timu zote zilitoka suluhu ya 0-0.
Mchezaji wa Prison Nurdin Chona akipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kidonda chake kuendelea kuvuja damu baada ya kugongana na mchezaji wa timu ya Simba Hamis Tambwe. |
Mchezaji Hamis Tambwe akipatia matibabu baada ya kujeruhiwa kwa kugongana na mchezaji wa Prison Nurdin Chona |
Kikosi cha Simba kilichopambana na Prison na kutoka suluhu ya 0-0 katika uwanja wa Sokoine leo jioni |
Kikosi cha Prison kilichokwaana na Simba leo jioni na kutoka suluhu ya 0-0 |
Benchi la Timu ya Simba |
Mashabiki wa timu ya Simba |
Mchezaji wa Simba Hamis Tambwe akiambaa ambaa na mpira huku mchezaji wa Prison Fred Chudu akiwa ameanguka chini |
Mchezaji wa timu ya Prison Nurdin Chona akipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuumia alipogongana na Hamis Tambwe |
Daktari wa Timu ya Simba akimpatia matibabu mchezaji wa timu hiyo Hamis Tambwe baada ya kujeruhiwa alipogongana na mchezaji wa Prison Nurdin Chona |
Wachezaji Awadhi Juma wa Simba na Omega Seme wa Prison wakiwa wameanguka chini baada ya kugongana walipokuwa wakiwania mpira |
Post a Comment