Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo asubuhi |
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria kikao na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya leo asubuhi |
TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA FEB-
2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN-
2014.
1. TATHMINI YA MAKOSA YOTE YA JINAI.
Katika kipindi
hicho cha Feb –2014 jumla ya makosa 2,003 yaliripotiwa, wakati kipindi kama
hicho mwezi Jan – 2014 makosa 2,438 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 435 sawa na asilimia 18.
2. TATHMINI YA MAKOSA MAKUBWA YA JINAI.
Katika kipindi
hicho cha Feb – 2014 jumla ya makosa
makubwa 196 yaliripotiwa, wakati
kipindi cha mwezi Jan-2014 makosa 212 yaliripotiwa, hivyo kuna pungufu ya makosa 16 sawa na asilimia 8.
3. TATHMINI YA MAKOSA YATOKANAYO YA JITIHADA
ZA JESHI LA POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA WADAU WENGINE.
Aidha
katika kipindi cha Feb – 2014 makosa makubwa yatokanayo na jitihada za Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali
katika kufanya doria,misako na operesheni katika kupambana na uhalifu na
wahalifu yaliripotiwa matukio 40, wakati
kipindi mwezi Jan- 2014 yaliripotiwa
makosa 56, hivyo kuna pungufu ya matukio 16, sawa na asilimia 29.
4. TATHMINI YA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI.
§ Kwa
upande wa makosa ya usalama barabarani jumla ya makosa/matukio yote
yaliyoripotiwa katika kipindi cha Feb –
2014 yakiwemo makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani na
usafirishaji ni 3,817 wakati kipindi
mwezi Jan- 2014 yaliripotiwa makosa 4,416 hivyo kuna pungufu ya makosa 599 sawa
na asilimia 14.
§ Matukio
ya ajali yaliyoripotiwa kwa kipindi cha Feb
– 2014 yalikuwa 29 wakati kipindi cha Jan-
2014 yalikuwa 38 hivyo kuna upungufu wa matukio 9 sawa na asilimia 24. Matukio ya ajali za vifo yaliyoripotiwa Feb – 2014 yalikuwa 15 wakati
kipindi cha Jan-2014 yaliripotiwa
matukio 27 hivyo kuna pungufu ya matukio 12 sawa na asilimia 44.
§ Watu
waliokufa kipindi cha Feb- 2014 walikuwa 18 wakati Jan -2014
walikuwa 30 hivyo kuna pungufu ya watu 12, sawa na asilimia 40.
Watu waliojeruhiwa kipindi cha Feb – 2014 walikuwa
watu 22 wakati Jan – 2014 walikuwa watu 49 hivyo
kuna pungufu ya watu 27 sawa na asilimia 55.
§ Katika
kipindi cha Feb - 2014 jumla
ya makosa 3,788 ya ukiukwaji wa
sheria za usalama barabarani na usafirishwaji yalitozwa faini sawa na tozo la Tshs 100,920,000/= ikilinganishwa na tozo la Tshs 131,340,000/= iliyokusanywa
katika kipindi Jan - 2014 kutokana
na makosa 4,378, hivyo kuna pungufu la kiasi cha tshs 30,420,000/= sawa na asilimia 23.
5.
MAJEDWALI KUONYESHA HALI YA UHALIFU.
MCHANGANUO WA MAKOSA
YOTE MAKUBWA YA JINAI NA USALAMA
BARABARANI KWA KIPINDI CHA FEB - 2014
IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JANUARI, 2014.
MAKOSA
|
FEB–
2014
|
JAN
– 2014
|
TOFAUTI +/-
|
ASILIMIA %
|
MAKOSA DHIDI YA BINADAMU
|
||||
MAUAJI
|
17
|
22
|
-5
|
-23
|
KUBAKA
|
36
|
44
|
-8
|
-18
|
KULAWITI
|
5
|
6
|
-1
|
-17
|
KUTUPA MTOTO
|
-
|
1
|
-1
|
-100
|
USAFIRISHAJI BINADAMU
|
3
|
-
|
+3
|
+300
|
JUMLA
|
61
|
73
|
-12
|
-16
|
MAKOSA DHIDI YA KUWANIA MALI
|
||||
UNYANG’ANYI WA K/SILAHA
|
1
|
2
|
-1
|
-50
|
UNYANG’ANYI WA K/NGUVU
|
13
|
9
|
+4
|
+44
|
UVUNJAJI
|
36
|
26
|
+10
|
+38
|
WIZI
|
291
|
440
|
-149
|
-34
|
WIZI WA PIKIPIKI
|
11
|
20
|
-9
|
-45
|
WIZI WA MIFUGO
|
18
|
15
|
+3
|
+20
|
JUMLA
|
370
|
512
|
-142
|
-28
|
MAKOSA DHIDI YA MAADILI YA JAMII
[YATOKANAYO NA JITIHADA ZA POLISI KWA USHIRIKIANO NA WADAU NA WANANCHI
MBALIMBALI]
|
||||
KUPATIKANA NA SILAHA
|
2
|
2
|
-
|
-
|
BHANGI
|
18
|
26
|
-8
|
-31
|
NYARA ZA SERIKALI
|
-
|
3
|
-3
|
-300
|
POMBE YA MOSHI.
|
17
|
15
|
+2
|
+13
|
WAHAMIAJI HARAMU
|
3
|
-
|
+3
|
+300
|
JUMLA
|
40
|
46
|
-6
|
-13
|
0.
MATUKIO YA USALAMA BARABARANI KWA KIPINDI
FEB - 2014 NA JAN 2014
|
||||
MATUKIO
|
3,817
|
4,416
|
-599
|
-14
|
MATUKIO YA AJALI
|
29
|
38
|
-9
|
-24
|
AJALI ZA VIFO
|
15
|
27
|
-12
|
-44
|
WALIOKUFA
|
18
|
30
|
-12
|
-40
|
WALIOJERUHIWA.
|
22
|
49
|
-27
|
-55
|
AJALI ZA MAJERUHI
|
14
|
11
|
+3
|
+27
|
MAKOSA YA UKIUKWAJI WA
SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA USAFIRISHAJI
|
3,788
|
4,378
|
-590
|
-14
|
TOZO [NOTIFICATION]
|
100,920,000/=
|
131,340,000/=
|
-30,420,000/=
|
-23
|
WITO WA KAMANDA:
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Z. Msangi
anatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa
taarifa sahihi na kwa wakati za wahalifu na uhalifu katika maeneo mbalimbali
ikiwa ni kwa ya ujumbe mfupi wa maneno, mazungumzo ya simu au kwa kufika moja
kwa moja kituo cha Polisi.
Halikadhalika
Jeshi la Polisi katika kuhakikisha linafanya kazi kwa karibu zaidi na wananchi,
tumeunda Vikosi Kazi [Task Forces] kwa ngazi ya Kata na Tarafa. Kwa takwimu za
sasa, Mkoa wa Mbeya una jumla ya Kata 218 na Tarafa 27. Kwa Kuzingatia Weledi
katika kutoa huduma bora kwa Wananchi, Jeshi la Polisi, limeweka Askari Kata katika
kila Kata ambaye anashilikiana kwa karibu zaidi na wananchi na Uongozi wa
Serikali ya Mtaa/Kijiji katika utoaji wa huduma. Sambamba na hilo, Jeshi la
Polisi kwa sasa lina Mkaguzi wa Tarafa katika kila Tarafa ambaye anafanya kazi
na kikosi chenye jumla ya askari wasaidizi wapatao 15. Lengo la Jeshi la Polisi
ni kuimarisha ulinzi na usalama na kuhakikisha linafanya kazi na Wananchi kwa
karibu zaidi ikiwa ni pamoja na kutambua maeneo yenye wahalifu/uhalifu na
kuyashughulikia kwa haraka.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya pia anatoa shukrani kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa
Mbeya kwa ushirikiano mkubwa wanaoonyesha kwa Jeshi la Polisi na kwa wananchi
kwa njia ya kuhabarisha umma.
Aidha anatoa
wito kwa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao ya uandishi wa
habari [media ethics] ili kuepuka kupotosha umma na kuleta machafuko nchini.
“Ni imani yetu kuwa vyombo vya habari vinapotumika vizuri yaani kwa kufuata na
kuzingatia maadili ya kazi ni matumaini yetu uleta mabadiliko na maendeleo kwa jamii
husika, ni wajibu wetu kufikisha ujumbe sahihi na kwa wakati, ni wakati wa
kuandaa vipindi vya kuelimisha jamii [educative programmes], vipindi vya
kuhabarisha [informative programmes], vipindi vya kuhabarisha na kuburudisha
[infortainment programmes] kwa lengo la kujenga misingi mizuri na imara zaidi
kwa jamii kwa ujumla hasa vijana na watoto.
Rai yangu kwa
wamiliki wa vyombo vya habari kujijengea tabia ya kufanya tathmini ya utendaji
wao ikiwa ni pamoja na kukusanya maoni kutoa kwa wasikilizaji. Pia ni vyema
kufanya jitihada za dhati kutanua usikivu wa matangazo ya vyombo vya habari
[media coverage] kwani kuna wananchi wengi wenye mahitaji ya kupata matangazo
sambamba na kupata elimu kupitia vyombo vya habari.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment