Ads (728x90)

Majira ya saa 6:30 adhuhuri Jumapili March 16 eneo la Kitonga mkoani Iringa magari yalishindwa kuendelea na safari kutokana na gari moja kupata ajali katikati ya Mlima Kitonga na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari yanayoenda na Dar na yale yanayoelekea mikoa ya Nyanda za Juu kusini ya Iringa, Songea na Mbeya.

Joto na jua kali lililokuwepo eneo hilo lilisabababisha baadhi ya abiri kushuka kwenye magari yao na kujisitiri chini ya vimvuli vya miti iliyop[o pembezoni mwa barabara hiyo kama wanavyoonekana pichani.
Baadhi yao walishindwa  kuhimili joto hilo lililoambatana na njaa na hivyo kulazimika kukaa chini ya mvungu wa gari ili kujisitiri na jua.

Hali ilipokuwa mbaya baadhi yao walilazimika kuhemea vyakula katika vijiji vya jirani na kuamua kuchukua majiko yao ya mkaa kwa ajili ya kuandaa msosi kama picha zinavyojidhihirisha.



Umati wa abiri walioshuka kwenye magari yanayokadiriwa kufika 1000 waendao na wale watokao Dar walishuka na kuhaha huku na kule bila kupata ufumbuzi wa safari yao.


Gari hili ndilo lililokuwa chanzo cha msongamano huo ambapo liligongana na gari jingine na kukatisha barabara hiyo iliyopo eneo la Kitonga ambalo ni maarufu kwa kuwa ni Mlima mrefu unawaogopesha madereva wengi wa magari wapitao eneo hilo.

Baada ya kugongana gari hilo lilikatisha njia na kuzuia magari yote yaliyokuwa yakielekea na kutoka Dar es salaam.

Baadhi ya wananchi walijityokeza kutoa msaada wa kulisukuma gari lililozuia barabara na kusababisha msongamano

Baadhi ya abiria walishindwa kuhimili joto kutokana na jua kali na kukata kiu kwa kunywa maji na juise kama anavyoonekana abiria huyu pichani


Msururu wa magari yalishindwa kuendelea na safari na hivyo kila gari lililofika eneo hilo lilijikuta likisimama kusubiri utaratibu  wa kuondoka eneo hilo


Hatimaye magari yalimudu kuodoka eneo hilo baada ya gari lililozuia njia kusukumwa ambapo majira ya saa 11:30 magari yalianza kuruhusiwa kuondoka eneo hilo kwa zamu huku mengine yakisubiri utaratibu wa kuruhusiwa.

Abiria waliokuwa wakieleeka Mbeya ambao waliondoka Dar es salaam kuanzia saa 12 alfajiri walijikuta wakiingia Mbeya majira ya kuanzia saa 4 hadi saa 5 usiku ilhali abiri waliokuwa wakielekea Dar kutokea mikoa ya Iringa, Mbeya na Ruvuma walijikuta wakiingia Dar kuanzia saa 6 hadi saa 8 usiku hali iliyosababisha wasafiri kwa zaidi ya saa 24 tofauti na kawaida ya kusafiri ndani ya saa 12 tu.

Post a Comment