Kijana wa Kiindonesia Dede Koswara akionekana baadhi ya viungo vyake vya mwili vikiwa vimeota vipande vya miti. |
Dede baada ya kupata maradhi |
Dede Koswara kabla hajaanza kugeuka mti maradhi yaliyosababisha mkewe kukimbia |
Pamoja na hali aliyonayo Dede alimudu kufanya shughuli zingine za kawaida kama vile kuandika na hata kula chakula mwenyewe kama anavyoonekana katika baadhi ya picha. |
Dede akipata chakula |
Anavyoonekana Dede kwa sasa baada ya kufanyiwa upasuaji
Dede akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji
Si Dede tu mwenye matatizo ya aina hiyo baadhi ya watu wengine wamekumbwa na aina hii ya maradhi na kuwa kama inavyoonekana picha hii kwa msaada wa mtandao |
Mwili wa Dede ukiwa na chunusi ambao ni ugonjwa unaoelezwa umetokana na kipande cha mti kumchoma katika mwili wake. |
''HUJAFA hujaumbika'' ni msemo wa Kiswahili unaoelezea tafsiri ya maisha ya kiumbe na maumbile yake halisi aliyoumbwa na Mwenyezi Mungu na baadaye kuishi duniani kwa kadri Mungu alivyomkadiria maisha yake.
Unaweza kuzaliwa ukiwa na viungo kamili vya mwili wako, lakini kutokana na mazingira ya maisha yanayotokana na tabia za kimaumbile viungo vya mwili wa binadamu vinaweza kubadilika na kuwa katika taswira nyingine tofauti na taswira ya awali ambayo umezaliwa nayo.
Aidha maumbile ya binadamu pia yanaweza kubadilika kutoka umbile moja hadi jingine kutokana na maradhi ama ulemavu unaotokea baadaye ambao si wa kuzaliwa.
Wapo wanaozaliwa na ulemavu wakaendelea kuishi nao hadi mwisho wa uhai wao na wapo wanaozaliwa wakiwa na maumbile kamili na baadaye mwisho wa uhai wao wakawa vilema wa viungo mbalimbali katika miili yao.
Wapo wanaozaliwa wakiwa wanaona vyema kwa mboni zao lakini baadaye wakapoteza uoni wao kutokana na mazingira mbalimbali wanayokutana nayo, pia wapo wanaopata ulemavu kutokana na maradhi na wengine kwa ajali.
Matukio haya kwa ujumla wake yanahitimisha msemo wa Hujafa hujaumbika ambapo kijana Dede Koswara(32) ambaye picha zake zimesambaa katika mitandao mbalimbali duniani anaonekana namna ambavyo anaishi kwa mateso kutokana na mwili wake kuota vipande vya miti kama inavyoonekana pichani.
Koswara mkazi wa Kijiji cha West Java nchini Indonesia amekuwa ni sehemu ya kivutio cha ajabu kutokana na mwili wake kuwa na maumbile yanayostaajabisha watu.
Kijana huyo ambaye ameanza kukutwa na matatizo hayo akiwa na umri wa miaka 15 wakati huo akiishi na mke na wanawe wawili anasimulia kuwa alipata kuchomwa na kipande kidogo cha mti mwilini mwake ambapo kiliendelea kukua taratibu hadi kufikia urefu wa sentimeta 5.
Hali duni ya kipato ilimsababisha kijana huyo kukosa matibababu na kusababisha mkewe kumkimbia na kumuachia watoto wawili.
Tatizo la Dede lilisikika kote duniani ambapo madaktari mabingwa walifika nchini humo kujaribu kuokoa maisha yake ambapo Daktari wa kimarekani alimfanyia utafiti Dede na kubaini kuwa alikuwa na ugonjwa ujulikanao kwa jina la 'Human Papilloma Virus' (HPV) unaosababishwa na vipande vidogo vya miti.
Taarifa zinaeleza kuwa Dede alipata kufanyiwa upasuaji nchini kwake mara kadhaa kwa ajili ya kumuondoa vipande vya miti vinavyoota mwilini mwake.
Daktari Siti Padilah Supari kwa kushirikiana na Daktari wa kutoka nchini Marekani walijaribu kumfanyia upasuaji mara tatu na kumpatia vidonge vya vitamin A vya Anti- Viral ambavyo huuzwa gharama kubwa ambapo taratibu hali ilianza kuonesha kuwa anaweza kurejea katika hali yake ya ubinadamu.(Kwa Msaada Wa Vyanzo Mbalimbali na Mtandao)
Post a Comment