Kila wanapoliona gari limeegeshwa wao hukimbilia wakiwa na ndoo za maji na vitambaa na kuanza kulisafisha bila mapatano na mwenye gari, akitokea mwenye gari humuonesha gari lake jinsi lilivyong'ara na kumuomba atoe chochote kutokana na kazi waliyoifanya, wengine hutoa elfu moja wengine mia tano, wengine hutoa mia mbili na wengine hawatoi chochote.
Wale wanaotoa chochote vijana hao hushukuru na kwa yule asiyetoa chochote hatimaye huambulia matusi kutoka kwa vijana hao jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wakazi wa jijini Mbeya, kwani kwanza kazi hiyo huifanya bila makubaliano.Kazi kwenu askari wa jiji la Mbeya.
Post a Comment