Waiona hiyo Mandhari yakhee!!!! huu ndio ufukwe wa zinjibari ulivyo kama unavyoonekana kupitia angani nyakati za Magharibi, ni mandhari inayovutia ambayo watalii kutoka nchi mbalimbali duniani hupenda kutembelea na kupunga upepo mwanana ulionakshiwa kwa rihi mwanana ya marashi ya Karafuu,Hii ndio Zinjibari au Zanzibar kama inavyozoeleka kupitia katika vinywa mbalimbali vya watu wa makabila tofauti.
Ni kisiwa kidogo lakini kilichobeba umaarufu wa aina yake Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla,ni miongoni mwa miji mikongwe iliyoasisi ustaarabu kabla ya kungia kwa wakoloni wa kijerumani na hata waingereza enzi hizo ikiwa chini ya utawala wa Sultani Seyyid Bin Sayyid.Aidha utawala huo pamoja na kuleta ustaarabu uligubikwa udhalili kwa wakazi wa miji ya Afrika ambao waliuzwa kama watumwa na kupelekwa nje ya nchi kutumikishwa kazi za sulubu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment