ambavyo anaamini kwa kutumia ufasaha wake jamii inaweza kujinasua kutoka hatua moja kuelekea hatua nyingine, aghalabu kauli fasaha ndiyo ambayo humfanya mtu kujua nini kinachozungumzwa katika jamii husika kiwe kiko katika mazingira aina yoyote iwayo kulingana na maudhui na mandhari ya eneo husika.
Muhimu hapa wote tuzigeze kauli zetu kifasihi ili iwe rahisi kwa jamii kujua nini kinachozungumzwa na iwe ni hatua ya kuweza kutafutiwa ufumbuzi wake, kwa lugha nyepesi jamii inaweza kueleweka nini kilichopo na nini mahitaji yanayohitajika kwa jamii husika na nini mustakabali wa jamii kwa kauli za kifasihi ambazo daima dawamu huzungumzwa na viongozi waliobeba dhima ya utawala badala ya kuongoza jamii.
Jamii imegeuka na kukubali kugeuzwa na kutawaliwa ilhali enzi za utawala zilipita karne dahari zilizopita, hivi sasa ni mmoja kuridhiwa na wananchi kuwa kiongozi wa wenzie au kuwa mchunga wa wenzie katika jahazi ambalo linapita katika mikondo ya maji pima ambayo ndani yake wapo Papa na Nyangumi ambao hutarazia kilichomo ndani ya Jahazi hili la Wadanganyika.
Tuwemo pamoja katika kutafakari mustakabali kwa lugha za KIFASIHI!!
Wakatabahu
Post a Comment