Imetokea katika mtaa mmoja katika jiji la Mbeya, ndege huyu alikuwa katika tafakuri yakinifu!!! kwamba Pamoja na kuthaminiwa na kulishwa pumba na punje za mahindi na mchele lakini hapa alipo anatafakari,kwani wageni wamefika nyumbani anasikilizia kwa dirishani!!!! kuwa hawa wageni wataondoka ama watalala, maana wakiamua kulala tu basi hapa kisu ni halali ya shingo yake, Mungu wangu viumbe wengine hufugwa ili watafunwe tu na binadamu, Ole wenu enyi binadamu mpendao kutafuna wenzenu iko siku nanyi mtageuzwa vitafunwa vya wengine>
Ndege Wawili
Ewe ndege wa thamani tulia mwako tunduni, usirukeruke mitini!!! utaingia mtegooni!!,RANGI yako ya kijaani na mwili wako laini!!!itunze yako thamani,watu wasikutamaaani, Ndege huyu ni mwandani, mwingine simthamini bali ni huyu wa ndaani!!aniridhishaye na kunithamini!!!!!Mhhh nilikuwa nakumbuka enzi zile za malenga!!! ujuzi hauzeeki, ajitokeze anaywejifanya malenga kama sijamtoa mkuku, kwa kuwa tumenyamaza!!!! vina na mizani vinapanda washikaji!!!!nimemfundisha huyu ndege wangu kuimba kila nikifika tu nyumbani huniimbia wimbo huu, waaaao!!!! Kasuku wangu ananiburudisha hata njaa huwa haiumi yaani nasahau hadi kula.
Post a Comment