Unamuona huyu mama hapa?unaiona hii ndoo ya Plastiki ya katikati? unaouona huo mstari mweusi katika ndoo hiyo?...Basi hiyo alama nyeusi ni namna ambavyo ndoo hiyo imechomwa ili kupunguzwa ukubwa kwa kubanwa na moto...ukinunua ndoo moja ya viazi ukivipima tena katika ndoo halisi, unapata nusu ya ndoo, usione hivyo viazi kama vimejaa katika hiyo ndoo, ndani yake hakuna kitu vimewekwa viazi vidogo vodogooo, Wauzaji hawa katika kijiji cha Ntokela barabara ya kuelekea Tukuyu kutokea Mbeya huwauzia wasafiri wanaokuwa katika mabasi na magari mengine, wanachokifanya ni kukununulia mfuko na kumimina viazi hivyo na kukufungia mzigo wako haraka haraka, wakati ukitafakari baada ya kumlipa gari hilooo nalo linaondoka maumivu unakuja kuyapata wakati umefika nyumbani kwako unamimina viazi kumbe ni nusu debe!!!!! Lahaula!!!! hii ni biashara au wizi, wako wapi watu wa viwango????
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wizi huu umekuwa ukifanywa na wafanyabiashara wengi sana hata maeneo ya Iringa sehemu ya Rungemba ,Ilula ,Morogoro pia ewananchi wanaibiwa kwa mtindo huu nafikiri sasa ni wakati umefika kwa wanahabari kusaidia kuelimisha umma ili kuepukana na hali kama hizi big up sana kwa kufichua wizi huo By Francis Godwin
ReplyDeleteNashukuru kwa kutembelea kijijini kwangu, mambo vp huko Ira kwa Wanyalukolo, vp wa2 wa Kijiweni, Mshindo, Kitanzini, Miyomboni, Makorongoni, Mlandege,Kihodombi, Kihesa, Mwangata,Wilolesi, Gangilonga wazima wote?unajua nimetaja mitaa hiyo ndiyo ambayo nilikuwa nacheza chandimu enzi hizoo nikiwa Primary.
ReplyDelete