Ads (728x90)



OFISI YA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA TEKU IKIWA IMEFUNGWA
 
WANAHABARI WAKIMSUBIRI MAKAMU MKUU WA CHUO KUTOA TAMKO JUU YA MGOMO WA WAHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA TEKU

WANAHABARI WAKIWA WAMEKAA MLANGONI KWA MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA TEKU KUSUBIRI TAMKO

BAADA YA KUSUBIRI KWA MUDA MREFU WANAHABARI WANALAZIMIKA KUANDIKA KIMEMO KWA MAKAMU MKUU WA CHUO ILI KUTOA TAMKO AMBALO AMEKUSUDIA KUTOA KWA WANAHABARI JUU YA MGOMO WA WAHADHIRI WA CHUO HICHO

HATA BAADA YA KUTUMA KIMEMO KWA MAKAMU MKUU WA CHUO HICHO BADO WANAHABARI WALIENDELEA KUSIMAMA MLANGONI, HUKU BAADHI YAO WAKIWA WAMECHOKA NA KUAMUA KUPUMZIKA KATIKA VITI
 
JITIHADA ZA KUPATA TAARIFA ZA WANAHABARI ZILIWAFIKISHA KWA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI AMBAYE HATA HIVYO ALISHINDWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WANAHABARI NA KUTOA MANENO YA MKATO KAMA VILE YEYE NI ZAIDI KWA KILA KITU, HAPA RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI AMBAO WANATARAJIA KUFANYA MTIHANI JULAI MOSI AKIWAACHA WANAHABARI SOLEMBA  NA KUTIMUA ZAKE

BAADHI YA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TEKU AMBAO HAWAJUI HATIMA YAO YA MITIHANI BAADA YA WAHADHILI WA CHUO HICHO KUTISHIA KUITSHA MGOMO

HATIMAYE BAADA YA SAA MBILI NA NUSU KAIMU MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA TEKU DKT. DANIEL MOSES ALIWAITA WANAHABARI NA KUZUNGUMZA MANENO MACHACHE KUWA MTIHANI UTAKUWEPO KAMA KAWAIDA JULAI MOSI NA JULAI MBILI NA KUKANUSHA TAARIFA ZA AWALI KWAMBA WAHADHIRI WA CHUO HICHO WAMEGOMA

KAIMU MAKAMU MKUU WA CHUO CHA TEKU DKT.DANIEL MOSES AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI KUSISITIZA KUWA UONGOZI WA CHUO UTAKAA NA WAHADHIRI KUMALIZA TOFAUTI ZILIZOPO TOFAUTI NA TAARIFA ZA AWALI ZILIZOTOLEWA KUWA WANAFUNZI HAWATAFANYA MTIHANI JULAI MOSI MWAKA HUU









Post a Comment