Ads (728x90)

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, BERNARD MEMBE
 

 


BAADHI YA WAHITIMU YA WANAZUONI WAHITIMU WA VYUO VYA TEKU NA MZUMBE WANAJUMUIYA WA KANISA KATOLIKI WAKIFUATILIA KWA MAKINI HOTUBA ZA VIONGOZIMJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC) SAMBWEE SHITAMBALA AKITETA JAMBO NA ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA MBEYA EVARIST CHENGULA


STORI NA RASHID MKWINDA
WAZIRI wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Bernard Membe ametoa angalizo kwa watu wanaohitaji msaada wa fedha kutoka kwa baadhi ya wanasiasa kuwa na tahadhari na fedha hizo kwa kuwa baadhi yake ni fedha ambazo zimetokana na ufisadi.
Kauli hiyo ya Bw. Membe ilitolewa kwa niaba yake na Mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa Bw. Sambwee Shitambala jijini Mbeya mwishoni mwa wiki kwenye ukumbi wa chuo kikuu cha TEKU huku kukiwa na wimbi la baadhi ya wanasiasa kutajwa kuwania kugombea urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2015.

Baadhi ya wanasiasa wanaotajwa kuwania urais kupitia CCM ni pamoja na Mbunge wa Monduli,Bw. Edward Lowassa,Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Samwel Sitta na Bw. Membe.

Akizungumza wakati wa mahafali ya Jumuiya wanafunzi wa katoliki elimu ya Juu MUCCASA jijini Mbeya Bw. Shitambala alisema kuwa yeye ametumwa kumwakilisha Bw. Membe katika mahafali hiyo ambapo alisema kuwa amewaagiza kuwa na tahadhari na fedha za baadhi ya wanasiasa wanaochangia makanisa.

Alisema kuwa kuna haja ya kuwa na vyanzo vya fedha halali ambazo zitatumika kihalali badala ya kuwa na fedha chafu ambazo zinatumika kwa kisingizio cha kutoa misaada katika taasisi mbalimbali za kijamii.

‘’Fedha chafu zisiingizwe kwenye mambo ya dini, tuwaangalie hawa wanasiasa wanaokuja na kumwaga fedha kwa kisingizio cha kusaidia jamii,’’alisema.

Awalin akizungumza na wanazuoni hao Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya Evarist Chengula aliwaasa vijana hao kutojiingiza katika migongano na migomo inayoweza kusababisha migogoro ya kijamii na kuhatarisha amani na utulivu wa nchi yetu.

Askofu Chengula alisema kuwa elimu waliyoipata itumike kwa maslahi ya Taifa ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu uliopo badala ya kujiingiza katika makundi ambayo yameonesha nia ya kuliingiza Taifa kwenye vurugu.

‘’Taifa linahitaji mchango wenu katika kudumisha amani na utulivu, nyinyi ni kundi kubwa le nye nguvu, mkitumika vizuri amani itapatikana, mkitumika vibaya, mtaliingiza Taifa letu kwenye majanga,’’alisema Askofu Chengula.

Post a Comment