Ads (728x90)

BAADHI YA VIONGOZI NA MASHABIKI WA TIMU YA NJOMBE MJI WAKIINUKA NA KUNIFUATA BAADA YA KUPIGWA PICHA WALIPOKAA NA WACHEZAJI WAO KWENYE BENCHI SIKU YA MECHI KATI YA TIMU YAO NA KIMONDO FC YA MBOZI

ILIKUWA NI WAKATI WA MAPUMZIKO AMBAPO TIMU ZOTE ZILIKWENDA KUPATA MAWAIDHA KUTOKA KWA VIONGOZI WAO, TIMU YA NJOMBE ILIBAKI KATIKA BENCHI LAO LA UFUNDI NA TIMU YA KIMONDO ILIINGIA VYUMBA VYA KUBADILISHA NGUO, KWANGU ILIKUWA NI FURSA YANGU KUWAAAAPIGA PICHA KWA KUWA PICHA ZA MWANZO W AMECHI NILIZIKOSA

LAKINI BAHATI MBAYA ZAIDI HAWA JAMAA WA TIMU YA NJOMBE MJI NI WA AINA YAKE WALIANZA KUNIPA KICHAPO BILA SABABU ZA MSINGI NA KUNIVUNJIA KAMERA YANGU, WALINIUMIZA!!!

HAPA JAMAA BILA AIBU ANARUSHA NGUMI HUKU JAMAA MWINGINE AKIVUTA KAMERA YANGU, ILIKUWA NI PATASHIKA HUKU BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WAKISHUHUDIA HATUA KWA HATU NAMNA AMBAVYO NILIKUWA NAPEWA KICHAPO!!

NILITAFAKARI MOYONI MWANGU, NA KUJIULIZA BAADA YA MASHBIKI KUSHUKA JUKWAANI NA KUNIVAMIA, KWAMBA HIVI IWAPO MMOJA WAPO ANGEKUWA NA SILAHA YOYOTE YENYE NCHA KALI ANGEAMUA KUNIDHURU LEO HII TUNGEKUWA TUNAZUNGUMZA LUGHA GANI?

JAMAA WALIENDELEA KUNIFANYA KAMA VILE MIE NI PUNCHING BAG WALIENDELEA KUNISHAMBULIA KADRI WALIVYOWEZA WAKATI HUO WOTE MIE NILIKUWA NAJITAHIDI KUOKOA KAMERA YANGU NA SEHEMU YANGU YA USO NISIJERUHIWE NA KUHARIBIWA SHAPE

HAPA JAMAA WALIENDELEA KUNING'ANG'ANIA KAMERA YANGU NAMI NIKIJITAHIDI KUIKOA

NILIENDELEA KUJITAHIDI KUJIOKOA PEKE YANGU KATIKA SAKATA HILI HUKU BAADHI YA WALIOKUWEPO WAKIOGOPA KULIVAA KUNDI HILI KUBWA LA WATU AMBAO WAMEJAA MAPEPO YA KISHETANI!!!

Post a Comment