Ads (728x90)

NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WADAU WOTE WALIOGUSWA JUU YA MKASA ULIONIKUTA WA KUPIGWA NA KUVUNJIWA KAMERA YANGU WAKATI WA MECHI YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KATI YA TIMU YA NJOMBE MJI NA KIMONDO FC, NI TUKIO LA KUSIKITISHA NA KUUMIZA ROHO KWA WALE WALIOANGALIA CLIP YA VIDEO NILIYOIWEKA MTANDAONI, JAMAA WALIWEKWA NDANI NA BAADAYE WALITOKA KWA DHAMANA, HATA HIVYO NILITAFAKARI KWA KINA TUKIO HILO NA MAKUSUDI YA MUNGU JUU YANGU, NIKAAMINI KUWA HUENDA MUNGU ALIKUWA NA MAKUSUDI YAKE KUNIPITISHA KATIKA JANGA HILI, INAWEZEKANA LINGEWEZA KUNIPATA KUBWA ZAIDI YA HILI, NIKAAMINI KUWA MUNGU KAWATUMIA HAWA JAMAA ILI IWE KAFARA YA BAADHI YA MAMBO AMBAYO NIMEWAHI KUMKOSEA MUNGU, KUTOKANA NA KADHIA YOTE NA MAUMIVU YOTE NILIYOYAPATA NATAMKA RASMI KUWA NIMEWASAMEHE, KWANI WALIONESHA KUJUTIA KOSA LAO NA ZAIDI YA YOTE WAMEFIDIA KAMERA YANGU IJAPOKUWA UWEZO WAKE NI MDOGO TOFAUTI NA KAMERA YANGU YA MWANZO, YOTE NIMEMTUPIA MUNGU NA NAMSHUKURU MUNGU KWA YOTE, NIKO NA MOYO SAFI KABISA NIMEWASAMEHE KUTOKA NDANI YA SAKAFU YA MOYO WANGU NA MUNGU NI SHAHIDI KWA HAYA NIYASEMAYO,NIMEMUOMBA MUNGU PIA KIZAZI CHANGU KISIJE KUJIKUTA KIKILIPIZA KISASI KWA HILI LILILONITOKEA, NDUGU, MARAFIKI NA JAMAA ZANGU, WACHUKULIE KUWA JAMBO HILI HUENDA LIMENITAKASA KWA DHAMBI AMBAYO SIIJUI NI LINI NIMEMKOSEA MUNGUPost a Comment