Ads (728x90)


WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKIPEANA MIKONO NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII, KABLA YA KUANZA KWA MECHI YA LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KATIKA UWANJA WA SOKOINE LEO JIONI

TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA-MARA

TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI-MBEYA

GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII  EMANUEL DAUD AKISHANGAA GOLI LILILOFUNGWA NA MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO CHARLES HIZA DK YA 12

GOLI LILIPITILIZA NA KUPENYA KWENYE NYAVU NA KUSABABISHA REFARII NA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MBEYA KUREKEBISHA NYAVU HIZO KWA DAKIKA KADHAA KABLA YA MPIRA HAUJAWEKWA KATI






Add caption




GOLI LA TATU KWA UPANDE WA KIMONDO BAADA YA MPIRA WA PENALT GOLI LILIFUNGWA NA MCHEZAJI LUKA MPOSHI DK 59

WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO WAKISHANGILIA GOLI




KIPUTE KINAENDELEA UWANJANI


PATASHIKA KATIKA GOLI LA POLISI JAMII


NDEREMO NA HOI HOI ZILITAWALA BAADA YA KIPYENGA CHA MWAMUZI KUPILIZWA HUKU KIMONDO FC IKIWA MBELA KWA MABAO 3-1

POLISI WALILAZIMIKA KUMTOA NJE YA UWANJA REFARII KUTOKANA NA KUZONGWA NA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII MARA BAADA YA KUMALIZIKA KWA MCHEZO


HOI HOI ZA FURAHA ZINAENDELEA

MASHABIKI WAKIWA WAMEMNYANYUA JUU MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK AMBAKISYE BAADA YA TIMU HIYO KUJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU TANZANIA BARA




SHANGWE NA HOI HOI ZINAENDELEA KATIKA DIMBA LA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MKOANI MBEYA



KOCHA WA TIMU YA POLIS JAMII MADENGE OMAR AKILALAMIKIA UTARATIBU WA UENDESHAJI WA LIGI HIYO

PONGEZI ZINAENDELEA

'TUMESHINDA TUNAMSHUKURU MUNGU TUMEPITIA VIGINNGI NA VIKWAZO VINGI'' AKIONEKANA ANASEMA MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK MINGA



SHABIKI WA TIMU YA KIMONDO MBEGU MOJA AKIWAZAWADIA WACHEZAJI WA TIMU HIYO SH. 200,000 BAADA YA USHINDI



TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI MKOANI MBEYA LEO IMEJIPATIA TIKETI YA KUCHEZA LIGI KUU BARAA BAADA YA AKUICHABANGA TIMU YA POLISI JAMII YA BUNDA MKOANI MARA BAO 3-1.

MCHEZO HUO WA LIGI YA MABINGWA WA MKOA ILIZIKUTANISHA TIMU HIZO KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINI JIJINI MBEYA IKIWA NI WA MARUDIANO BAADA YA MCHEZO WA AWALI ULIOCHEZWA MKOANI MARA KUTOKA SULUHU YA MABAO 2-2.

TIMU YA KIMONDO ILIANZA KUONA NYOTA NJEMA KATIKA DAKIKA YA 12 YA MCHEZO BAADA YA MSHAMBULIAJI WA TIMU HIYO CHARLES HIZA KUPOKEA PASI KUTOKA KWA JOFREY MLAWA NA KUPIGA SHUTI ILIYOJAA KIMIANI NA KUMUACHA GOLIKIPA WA TIMU YA POLISI JAMII EMANUEL DAUDI AKISHANGAA GOLINI.

BAADA YA GOLI HILO KULIKUWA NA MASHAMBULIZI YA HAPA NA PALE KATIKA GOLI LA POLISI JAMII AMBAPO DAKIKA TANO BAADAYE TIMU YA KIMONDO ILIJIPATIA GOLI LA PILI LILILOFUNGWA KWA KICHWA NA MCHEZAJI COSMAS MWAZEMBE.

BAADA YA KUFUNGWA FOLI HILO TIMU YA POLISI JAMII ILIAMKA KUTOKA USINGIZINI NA KUFANYA MASHAMBULIZI KATIKA GOLI LA KIMONDO AMBAPO MASHAMBULIZI HAYO YALIZAA MATUNDA DAKIKA YA 30 BAADA YA MSHAMBULIAJI WA TIMU YA POLISI JAMII JOSEPHAT ONYANGO KUIPATIA TIMU YAKE BAO LA KUFUTIA MACHOZI.

HADI TIMU ZINAENDA MAPUMZIKO MABAO YALIKUWA NI 2-1, KIPINDI CHA PILI KILIANZA KWA MASHAMBULIZI YA HAPA NA PALE AMBAPO TIMU YA POLISI JAMII ILIONEKANA KUZIDIWA UWEZO NA TIMU YA KIMONDO BAADAA YA MPIRA KUCHEZWA NUSU UWANJA KWA TAKRIBANI DAKIKA 15.

MASHAMBULIZI YA TIMU YA KIMONDO KWA TIMU YA POLISI JAMII YALISABABISHA KUFANYIKA MADHAMBI KATIKA GOLI LA TIMU YA KIMONDO BAADA YA MCHEZAJI WA TIMU YA POLISI JAMII KUMCHEZEA FAULO MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO  CHARLES HIZA NA HIVYO KUSABABISHA REFARII KUTOA PENALT AMBAPO MCHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO LUKA MPOSHI ALIFUNGA GOLI LA TATU KATIKA DAKIKA YA 59 YA MCHEZO.

HADI KIPENGA CHA MWISHO KINAPULIZWA KIMONDO ILIKUWA INAONGOZA KWA MABAO 3-1.

KUTOKANA NA MCHEZO HUO TIMU YA KIMONDO IMEJIHAKIKISHIA KUCHEZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA AMBAPO TIMU YA POLISI JAMII INATAFUTA NAFASI YA TATU.

Post a Comment