Ads (728x90)

PICHA HIZI ZINAONESHA JINSI MASHABIKI NA VIONGOZI WA TIMU YA NJOMBE WALIVYOTEKELEZA AZMA YAO YA KUNIPIGA NA KUNIVUNJIA KAMERA YANGUJUMAPILI, JUNI 2 NI MOJA KATI YA SIKU AMBAYO SITAISAHAU KATIKA KUMBUKUMBU ZANGU ZA KAZI ZA HABARI, NI SIKU AMBAYO IMENIINGIZA KATIKA HISTORIA NISIYOITARAJIA HATA KUFIKIA HATUA YA KUONA KUWA KUNA HAJA YA WANAHABARI KUANZA KUTUMIA NGUVU YA ZIADA KWA AJILI YA KUJILINDA KILA WAKATI WANAPOKUWA KAZINI.
NIKIWA KATIKA MAJUKUMU YANGU YA KAWAIDA KAMA ILIVYO DESTURI, SIKU HIYO NILISHINDA NYUMBANI KUANZIA ASUBUHI NIKIJISHUGHULISHA NA MAJUKUMU YA KILA SIKU YA KUIHUDUMIA FAMILIA YANGU, ILIPOTIMU MAJIRA YA SAA KUMI NILIMUITA MWANANGU WA KIUME ANAYESOMA KIDATO CHA PILI, ILI NIAMBATANE NAYE KATIKA MECHI YA MPIRA WA MIGUU KATI YA TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI MBEYA NA NJOMBE MJI YA MKOANI NJOMBE.
BAHATI MBAYA KIJANA WANGU HUYU WA KIUME ALIKUWA HAJAJIANDAA KWANI MUDA WOTE ALIKUWA KATIKA SHUGHULI ZA KUWASAIDIA WADOGO ZAKE KAZI ZA NYUMBANI, HIVYO ILIMLAZIMU KUBAKI KWA KUWA KUJIANDAA KWAKE KUNGESABABISHA NICHELEWE KURIPOTI MECHI HIYO.
NAAMINI KUBAKI KWAKE NYUMBANI KUMESAIDIA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE KWANI ANGESHUHUDIA PICHA AMBAYO KAMWE ISINGEONDOKA KICHWANI MWAKE.
MWANANGU ANGESHUHUDIA NAMNA AMBAVYO NAPOKEA KIPIGO KUTOKA KWA WANANCHI AMBAO SIKU ZOTE WANATEGEMEA MSAADA WA WANAHABARI KATIKA MAMBO YAO YA KILA SIKU HUSUSANI KATIKA MCHEZO WA MPIRA.
MWANANGU ANGESHUHUDIA NAMNA AMBAVYO WATU HAO WAKINIPIGA KWA MATEKE NA MANGUMI NA KUNINYANG'ANYA KAMERA YANGU NA KUIVUNJA AMBAYO SIKU ZOTE NINAPOONDOKA KWENDA KAZINI ANANIKUMBUSHA KWA KUSEMA BABA UMESAHAU KAMERA YAKO CHUMBANI, ANAFANYA HIVYO AKIAMINI KUWA NDIYO INAYOMFANYA APATE KARO YA SHULE,INAYOMFANYA APATE FEDHA ZA MATUMIZI YA KILA SIKU ANAPOKUWA SHULENI,NDIYO ANAYOAMINI KUWA BILA HIYO BABA YAKE SINA UJANJA WA KUPATA FEDHA KWA NJIA NYINGINE.
NAFIKIRIA NAMNA AMBAVYO MWANANGU ANGEKUWA ANALENGALENGA MACHOZI WAKATI AKINISHUHUDIA KUNDI KUBWA LA WATU WANAOFIKIA 15 WAKINISHAMBULIA MIMI MTU MMOJA,KUTOKANA NA UMRI WAKE NAAMINI ANGEPATA HASIRA NA HATA KUFIKIRIA KULIPA KISASI, KUTOKANA NA MADHILA AMBAYO ANGESHUHUDIA NIKIYAPATA.
NAMSHUKURU MUNGU NILIMUACHA MWANANGU NADHANI MUNGU ALIONA KITAKACHOTOKEA UWANJANI, MWANANGU ANGEATHIRIKA KISAIKOLOJIA, ANGEUMIA SANA KUONA BABA YAKE NAPIGWA BILA KOSA, ANGEAMBUKIZWA TABIA HII YA KINYAMA INAYOFANYWA NA WATU,. ANGERITHI HII TABIA KWA KUAMBUKIZWA HASIRA NAAMINI KATIKA MOYO WAKE ANGEAMBUKIZWA CHUKI NA HATA KUFIKIRIA KULIPIZA KISASI, MUNGU AMEMUEPUSHIA.
SIKU HIYO KAMA NILIVYOELEZA AWALI NILIINGIA UWANJANI KWA KUCHELEWA NA KITU CHA KWANZA NILICHOKIFANYA BAADA YA KUINGIA UWANJANI NI KWENDA KWENYE MEZA YA MWAMUZI WA AKIBA NA KUOMBA LINEUP YA TIMU ZOTE MBILI, NILINAKILI FASTAFASTA MAJINA YA TIMU HIZO MBILI KWA KUYAPIGA PICHA KWA KUTUMIA KAMERA YANGU, KISHA NIKAONGOZA NA KWENDA KATIKA UPANDE WA GOLI KASKAZINI AMBAKO TIMU YA NJOMBE MJI ILIKUWEPO NILIKAA KONA YA KIBENDERA CHA UPANDE WA MAGHARIBI AMBAKO NILIREKODI MATUKIO YA MECHI HIYO HADI WAKATI WA MAPUMZIKO.
WAKATI WA MAPUMZIKO NILIELEKEA  KWENYE BENCHI AMBALO MARA ZOTE WANAHABARI HUKETI, KABLA SIJAFIKA KATIKA BENCHI HILO NILIWAONA WACHEZAJI WA TIMU YA KIMONDO FC YA MBOZI, MBEYA WAKIKIMBILIA KATIKA VYUMBA VYA KUBADILISHA NGUO, NILIJARIBU KUWAKIMBILIA ILI NIPATE PICHA YAO NIKACHELEWA, NIKAANGAZA UWANJANI NIKAWAONA WACHEZAJI WA TIMU YA NJOMBE MJI WAKIWA BADO WAKO UWANJANI, NIKAONA NI FURSA PEKEE YA KUWAPIGA PICHA WAKATI WANATOKA UWANJANI, NILIPATA PICHA KADHAA, BAADAYE NIKAWAONA WACHEZAJI HAO WAKIKETI KATIKA BENCHI LA UFUNDI LA TIMU YAO, NIKASOGEA UMBALI WA KAMA MITA 50 NIKAWAPIGA PICHA WAKIWA WANAPOKEA MAWAIDHA KUTOKA KWA VIONGOZI WAO.
GHAFLA NIKIWA NAWAPIGA PICHA GOLIKIPA WA TIMU HIYO ALIINUKA NA KUANZA KUNITUKANA MATUSI YA NGUONI, NILITAHARUKI KWA KITENDO HICHO KWANINI KIJANA HUYU ANANITUKANA MATUSI YA NGUONI, NIKASHIKWA NA KIGUGUMIZI KIDOGO NA KUTAFAKARI UDHALILISHAJI WA KIJANA YULE AMBAYE KWA UMRI ANAFANANA KABISA NA MWANANGU, GHAFLA FIKRA ZANGU ZIKANIKUMBUSHA KUWA PALE NILIKUWA KAZINI, NIKARUDISHA FIKRA ZANGU KATIKA KAZI ILIYONIPELEKA PALE, HIVYO KITENDO KILE CHA KUNITOLEA MATUSI YA NGUONI NA KUNINYOOSHEA MIKONO YA KUNISHAMBULIA NIKAKIWEKA KATIKA KUMBUKUMBU KATIKA KAMERA YANGU, MAYOWE YA KIJANA YULE YALIAMBUKIZA WACHEZAJI WENGINE AMBAO NAO WALIANZA KUNISHAMBULIA KWA MATUSI NA KUNINYOOSHEA VIDOLE NA MIKONO, NAMI SIKUIJALI HIYO HALI NIKAENDELEA KUPIGA PICHA ZA TUKIO HILO,BAADAYE MAYOWE YA WACHEZAJI HAO YALIWAAMBUKIZA VIONGOZI WAO, WALIINUKA KWA PAMOJA VIONGOZI NA WACHEZAJI WALIOKUWA WAMEKETI KATIKA BECHI LA UFUNDI LA TIMU HIYO NA KUNIFUATA NILIPO, NAMI NIKAWA NARUDI NYUMA ILI NIPATE VIZURI PICHA ZAO, WALINIFUATA KWA HARAKA NA KUNIVAMIA KWA UMOJA WAO, WAKINIPIGA KWA MATYEKE NA NGUMI, SIKUTETEREKA KUANGUKA CHINI BALI NILIJIKINGA KWA MGONGO WANGU NIKIIZUIA KAMERA YANGU HUKU, NGUMI NA MATEKE YA WATU WALE YAKITUA KATIKA MGONGO WANGU, KUNDI KUBWA LA MASHABIKI WA TIMU HIYO WALITOKA JUKWAANI NA KUJA KUJA KUNISHAMBULIA, NAMI NIKIENDELEA KUJIHAMI KWA KADHIA ILE.
FIKRA ZA UPWEKE ZILITAWALA KICHWANI MWANGU, NIKAANGAZA HUKU NA KULE KUHITAJI MSAADA KATIKA ENEO LILE AMBALO SIKU ZOTE TUMEZOEA KUONA NI ENEO LA STAREHE NA FURAHA, BAHATI MBAYA LEO HII LIMEGEUKA UWANJA WA VITA, NASHAMBULIWA! KISA NIKO KAZINI, NIKAJIULIZA, MOYONI MWANGU, INAWEZEKANA HAWA JAMAA NI KUNDI FULANI LA WAHUNI AMBAO STAREHE KWAO NI VURUGU.
NIKIWA KATIKA TAFAKARI HIYO, NIKAMUONA MWANDISHI MMOJA WA KIKE ANAITWA AINESI AKIJA HUKU AMEFURA KWA HASIRA AKAOKOTA KIPANDE CHA LENSI YA KAMERA YANGU AMBAYO ILIKUWA IMEDONDOKA CHINI WAKATI MMOJA WA MASHABIKI WA TIMU HIYO ALIKUWA AKIKIMBILIA KUTAKA KUIKANYAGA,NILIMUONEA HURUMA DADA HUYU KWANI ALIHAMAKI KWA HASIRA, NILITAFSIRI FIKRA ZAKE MACHONI MWAKE AKIONEKANA KAMA MTU ALIYETAMANI AWAVAMIE WAVAMIZI WALE NA KULIPIZA KISASI, MASKINI DADA HUYU ALICHUKUA KITAMBAA CHAKE NA KUNIFUTA VUMBI HUKU AKINIPA POLE,KIJANA MWINGINE MWANDISHI WA HABARI WA REDIO BARAKA FM LAUDENCE SIMKONDA NAYE ALIFIKA ENEO LILE AKANIOKOTEA NOTEBOOK YANGU NA KOFIA AMBAYO ILIDONDOKA CHINI WAKATI JAMAA HAO WAKINISHAMBULIA,BAADAYE ALIJITOKEZA RIPOTA MMOJA WA REDIO CLOUDS FM SALEHE KUPAZA AMBAYE ALIFIKA PALE NAYE AKIWA AMESHIKWA NA HASIRA, KWA MBALI NILIMUONA MMOJA WA VIONGOZI WAPENDA MICHEZO DT WA WILAYA YA MBOZI, BW. MBEGU MOJA AKIJA KWA KASI NA KUOKOTA KIPANDE KINGINE CHA KAMERA KILICHODONDOKEA UPANDE MWINGINE, HUKU UPANDE WA MAGHARIBI MWA GOLI LA UPANDE WA KUSINI AKIWA AMESIMAMA KOCHA WA TIMU ILIYOPANDA DARAJA YA MBEYA CITY, JUMA MWAMBUSI AKIWA NA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA MBEYA JUMA IDD, WAKIHAHA KUWAPIGIA SIMU POLISI ILI WAFIKE UWANJANI KUTOKANA NA TUKIO LILE.
BAADAYE NIKAWAONA BAADHI YA VIONGOZI WA TIMU YA KIMONDO, MWENYEKITI WA TIMU HIYO ELICK AMBAKISYE NA BAADHI YA MASHABIKI WA TIMU HIYO WAKIJA KUNIPA POLE KUFUATIA TUKIO HILO, BAADA YA DAKIKA 20 MAGARI MAWILI YA POLISI YALIFIKA UWANJANI HAPO, NIKAINGIA KATIKA GARI YA POLISI NA KUELEKEA CENTRAL POLISI.
AWALI KABLA YA KUINGIA KATIKA GARI LA POLISI TULITOKA MLANGO WA NYUMA AMBAKO KUNA BAADHI YA VIONGOZI WA TIMU YA NJOMBE WALIDAIWA KUTAKA KUKIMBIA BAADA YA KUONA ASKARI POLISI WAMEFIKA UWANJANI,JAMAA HUYU AMBAYE ANATEMBELEA GONGO KUTOKANA NA MGUU WAKE MMOJA KUWA NA HITILAFU NILIMKUTA MBELE YA GETI KUBWA LA KUINGILIA UWANJANI AKIWA AMESIMAMA NA ASKARI MMOJA NA JAMAA MMOJA MWANASHERIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BASIL.
MAZUNGUMZO YA WAKTI ULE HAYAKUWA NA TIJA KWANI KILA MMOJA WETU ALIKUWA KATIKA TAHARUKI HASA MIMI AMBAYE KWA WAKATI HUO NILIJIHISI MAUMIVU KATIKA MWILI WANGU KUTOKANA NA KIPIGO NILICHOKIPATA KUTOKA KWA MASHABIKI WAKATI NIKIJIHAMI NA KUOKOA KAMERA YANGU ISIVUNJWE.
BAADAYE NIKARUDI UWANJANI NA KUINGIA KATIKA GARI LA POLISI, KABLA YA KUELEKEA CENTRAL POLISI TULIZUNGUKA KATIKA MITAA YA UZUNGUNI HUKU BAADHI YA ASKARI WAKIMFUATILIA MMOJA WA MASHABIKI WALIOSHIRIKI KATIKA KWENYE VURUGU ZILE, TUILIZUNGUKA NA GARI UPANDE WA UZUNGUNIO NA BAADAYE TUKAELEKEA NJIA YA ISANGA KISHA ASKARI WALIKATA SHAURI WANIFIKISHE MIMI POLISI ILI NIKAANDIKISHE MAELEZO HUKU WAKIENDELEA KUWAFUATILIA WAHUSIKA WA VURUGU ZILE.
NILIFIKA KITUO CHA POLISI NIKIWA KATIKA TAHARUKI JUU YA MASAHIBU HAYA YALIYONIKUTA, NIKATAFAKARI AZMA YA WALE WATU KUNIVAMIA MIMI MTU MMOJA NA KUNIFANYIA VURUGU ILE.BAADA YA MUDA MFUPI WAKATI NIKIENDELEA KUANDIKISHA MAELEZO YANGU KITUO CHA POLISI ALILETWA MMOJA WA VIONGOZI WA TIMU YA NJOMBE AMBAYE ANATEMBELEA GONGO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ERASTO MPETE.
MPETE ALIAMRISHWA KUPITA MBELE YA KAUNTA YA POLISI NA KUAMRIWA KUKAA CHINI NA KUVUA VIATU, MACHO YA KUOMBA MSAADA YALIONEKANA DHAHIRI KATIKA SURA YA JAMAA HUYU AKIONESHA DHAHIRI KUJUTIA KILE KILICHOTENDEKA UWANJANI, LAKINI MAJUTO YALIKUWA NI MJUKUU, JAMAA YULE ALIFIKIA HATUA YA KUTAKA KUNIANGUKIA KUNIOMBA MSAMAHA KWA KILE KILICHOFANYIKA.
MOYO FULANI ULINISUKUMA KUMUONEA HURUMA LAKINI MOYO MWINGINE ULIKATAA NA GHADHABU ILINIPANDA NIKIMUANGALIA YULE JAMAA KUWA NI ADUI NAMBA MOJA AMBAYE ALIDHAMIRIA KUNIDHURU BILA KOSA LOLOTE. 

Post a Comment